Charles James, Michuzi TV
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Chamwino, Edson Sweti amesema kufuatia kifo cha Rais Dk John Magufuli, Taifa limempoteza Kiongozi Shupavu aliyeipenda Nchi yake akijitolea akili, moyo na nguvu zake katika kuwatumikia.
Sweti amesema kwa wananchi wa Wilaya ya Chamwino wamempoteza mkazi mwenzao kwani Rais Magufuli alikua anaishi Ikulu ya Chamwino.
Amesema kwa miaka mitano na miezi takribani mitatu ya uongozi wake amefanya mambo makubwa kwa Nchi huku wao kama Wilaya ya Chamwino pia wakinufaika kwa kiwango kikubwa na uongozi wa Rais Dk Magufuli.
" Wilaya ya Chamwino tuna sababu kubwa za kumshukuru Rais Magufuli ndio maana imetuuma sana, kwa niaba ya Halmashauri yangu natoa pole nyingi sana kwa Makamu wa Rais Mama Samia, Familia na watanzania kwa ujumla, niwaombe tushikamane katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Ndani ya miaka mitano Rais Magufuli ametufanyia maendeleo makubwa watu wa Chamwino katujengea Hospitali ya Uhuru yenye hadhi kubwa na vifaa vya kisasa, katujengea Hospitali ya Wilaya ya Mloa, amejenga miundombinu ya Maji na Barabara lakini tu kuifanya Dodoma kuwa Jiji ni zawadi kubwa katuachia," Amesema Sweti.
Amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwatumikia watanzania kwa uzalendo kwenye muda wake wa uongozo ikiwa ni pamoja na kukuza nidhamu kwa watumishi serikali jambo ambalo anaamini litaendelea kudumishwa ili kumuenzi.
" Shujaa wetu hajafa, amelala tu. Tutamuishi Dk Magufuli kupitia miradi yake mikubwa aliyotuachia, Mradi wa Umeme wa Mwalimu Nyerere, Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Ndege, Barabara na kutuachia uchumi ulio madhubuti uchumi wa kati," Amesema Sweti.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chamwino, Edson Sweti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...