Bendi maarufu ya muziki wa dansi The Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani, wamepokea kwa masikitiko na uchungu mkubwa msiba wa kifo cha Rais John Pombe Magufuli.
 
Kiongozi wa bendi hiyo mwanamziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja kwa niyaba ya bendi yake anatoa pole kwa Rais mpya Mama Samia Suluhu Hassan,pole kwa mama Janet Magufuli na familia yake na pole kwa watanzania wote. 
 
Bendi ya Ngoma Africa band inaungana na watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na kiongozi wetu Rais Magufuli ambaye alikuwa kipenzi chetu na rais aliyejitoa muhanga kwa ajili ya wanyonge. Ngoma Africa Band inaungana na watanzania katika maombolezo ya msiba huu.
 
Mungu ampumzishe Peponi Kiongozi wetu Hayati Rais John Pombe Magufuli - Ameen
MUNGU IBARIKI TANZANIA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...