
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Muuguzi
Mkuu Pemba Daktari.Omar Juma Ali akitowa maelezo ya Kituo cha Afya
kilichoko katika eneo hilo la Nyumba za Maafa Tumbe, Wilaya ya Micheweni
Mkoa wa Kaskazini Pemba, alipofanya ziara kutembelea Mradi huo.(Picha
na Ikulu)
BAADHI ya Nyumba za Maafa katika
Kijiji cha Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba
zilizojengwa kwa ajili ya Wananchi watakaopata na maafa Kisiwani
Pemba.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wa Kijiji cha Tumbe
Wilaya ya Micheweni wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani)
akizungumza na Wananchi hao katika viwanja vya Nyumba za Maafa Tumbe
alipofika kutembelea ujenzi huo.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wa Kijiji cha Tumbe
wakishangilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia
katika viwanja vya Nyumba za Maafa Tumbe Wilaya ya Micheweni alipofika
kukagua Mradi huo.(Picha na Ikulu) MZEE
wa Kijiji cha Tumbe Shehia ya Magharibi Bw.Juma Kombo Dadi akimsikiliza
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein
Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Tumbe
wakati alipofika kuangalia maendeleo ya Ujenzi wa Nyumba za Maafa Tumbe
Wilaya ya Micheweni Pemba, akiwa amebeba bago la picha za Waasisi wa
Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...