RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitembelea Kiwanda
cha Sukari Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja akiwa katika ziara yake
akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho Ndg. Rahim
Bhaloo (kushoto kwa Rais) akitowa maelezo ya uzalishaji wa sukari na
(kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed
Mahmoud na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar
Said Shabaan.(Picha na Ikulu) RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali
Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Ndg.
Rahim Bhaloo (kushoto kwa Rais) akitowa maelezo ya uzalishaji wa Sukari
katika kiwanda hicho wakati akiwa katika ziara yake leo na (kulia kwa
Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud,
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said
Shabaan na Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Mhe.Dkt.
Soud Nahoda Hassan.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Zanzibar,Ndg Rahim Bhaloo,
wakati wa ziara yake kutembelea kiwanda hicho kuangalia uzalishaji wa
sukari.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo na
kuangalia Sukari iliozalishwa na kiwanda hicho kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu Ndg. Rahim Bhaloo, akiwa katika ziara yake kujionea uzalishaji wa
Sukari kiwandani hapo leo, 6-3-2021.(Picha na Ikulu) MFANYAKAZI
wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Ndg. Amour Juma akitowa changamoto
zinazowakabili katika Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda, wakati
ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.
Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) mkutano huo umefanyika katika
viwanja vya kiwanda hicho Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja leo
6-3-2021.(Picha na Ikulu)
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali
Mwinyi akizungumza na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari na Wakulima wa
miwa, wakati wa ziara yake kutembelea kiwanda hicho kujionea uzalishaji
wa Sukari kiwandani hapo.(Picha na Ikulu)
MKULIMA wa zao la Miwa kutoka
Cheju Ndg.Mohammed Omar akizungumza changamoto zao kuhusiana kilimo cha
miwa wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) mkutano huo
umefanyika katika viwanja vya kiwanda hicho mahonda leo 6-3-2021.(Picha
na Ikulu) RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali
Mwinyi akisikiliza changamoto za Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari
Mahonda wakati wa ziara yake kutembelea kiwanda hicho leo 6-3-2021 na
(kushoto kwa Rais) Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Ndg.
Rahim Bhaloo.(Picha na Ikulu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...