Charles James, Michuzi TV
KATIKA maadhimisho ya wiki ya maji serikali inatarajia kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maji 281 yenye thaman ya Sh Trilioni 1.04.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na katibu mkuu wizara ya mhandisi Antony sanga wakati akizungumza na waandishi wa habari, alisema maadhimisho hayo yanatarajia kufanyika kuanzia machi 16 hadi 22 mwaka huu.
"Lengo la kufanya uzinduzi wa miradi hii katika kipindi cha wiki ya maji nikutumia fursa hiyo kuonyesha kwa vitendo mafanikio katika sekta ya maji na namna ambavyo huduma ya maji safi na usafi wa mazingira umeweza kuboreshwa na kuwafikia wananchi wengi zaidi," Amesema.
Mhandisi Sanga amesema katika wiki ya maji kutafanyika shughuli za upandaji wa miti katika vyanzo vya maji kuhabarisha na kuhamasisha wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji .
Amesema katika maadhimisho hayo nchi itaungana na mataifa mengine duniani kutathimini utekelezaji,mafanikio na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maji .
"Kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu ni Thamani ya maji kwa uhai na maendeleo, ambayo itasaidia kusimamia rasilimali za pamoha na utoaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira nchini," Amesema.
Katibu mkuu huyo amewataka wananchi kutumia wiki ya maji kupata elimu namna bora ya utunzaji wa vyanzo vya maji na kutoa changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...