NA  YEREMIAS  NGERANGERA….NAMTUMBO.

Mpenzi   wa timu  ya simba  Ally  Rashidi  Kuntika (71)katika  mamlaka ya  mji mdogo  wa Namtumbo  mkoani  Ruvuma  alidondoka  ghafla  na kufariki  dunia  papohapo  mara  baada ya  mchezaji wa timu ya  Simba   Chris  Mugalu  kukosa  kufunga  goli la penati  dhidi  ya timu ya Tanzania  Prison  .

 Afisa  mtendaji  mkuu  wa mamlaka ya  mji mdogo wa Namtumbo  bwana  Geofrey  Kalikawe alisema  marehemu alikutwa  na umauti  huo akiwa  katika kibanda  umiza  kwa  mzee kikoti akiangalia mpira  kati ya timu ya simba na timu ya Tanzania  Prison na mara baada ya timu ya simba  kupata penati  alionekana kuwa na furaha  isiyo  na kifani.

Kalikawe  alidai  marehemu  alikaa katika benchi  akiwa na watazamaji wengine  wakati  wanasubiri  mchezaji wa simba kupiga mpira wa penati  dhidi ya timu ya Tanzania Prison palikuwa na mabishano ya hapa na pale wengine wakidai anakosa  na  yeye akidai  hawezi kukosa .

Kitendo  cha mchezaji wa  Simba  kukosa kufunga penati hiyo  marehemu  aliinama  kwa muda mrefu na baada  ya watazamaji wengine waliokuwa wakishangilia  kukosa  kufungwa kwa goli  hilo walisogea kwa marehemu ili kumdhihaki  lakini walipofika kwake walikosa ushirikiano baada ya kudhania kuwa amezimia  na katika harakati za kuokoa maisha yake  wakagundua amefariki  dunia.

Kwa mujibu  wa mtoto wa marehemu Barakati  Ally  kuntika  alisema baba yake amefariki  dunia  wakati anatazama  mpira  katika kibanda  umiza kwa William Enas Kikoti  kwa kuwa  mzee wao alikuwa mpenzi  wa timu ya Simba kindakindaki  na kwa kuthibitisha  hilo alidai baba  yake aliwahi kutoa mbuzi( beberu)wakati timu ya  simba ilipokuwa inapita  namtumbo kuelekea  songea kucheza na timu ya majimaji kupitia njia ya Lindi na amewahi kuvunja redio baada ya timu ya simba kufungwa na timu ya Yanga siku za nyuma.

Mashabiki  wa timu ya Simba katika mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo akiwemo  Charles  Mkandawile  na  Moses  Bakari  walidai wamempoteza mpenzi  na shabiki wa kweli  wa timu ya simba ambaye  alikuwa  anashikilia msimamo wake wa kuipenda simba  hata wakati ule simba inafanya vibaka katika ligu kuu  yeye  alionekana kuitetea  Simba  kwa hali na mali na kumpatia mtoto wake wa kiume jina la kichuya.

Marehemu  atazikwa katika  makaburi ya Namtumbo kati ambapo ameacha wanawake 3,watoto 17 wakiwa wanawake 9 na watoto wa kiume 8 .

 

 MAREHEMU wakati wa uhai wake akiwa na mtoto wake wa kike nje ya nyumba yake

 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...