Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
Klabu ya Simba imeambulia sare ya bao 1-1 baada ya kusawazisha dakika za lala salama dhidi ya Maafande wa Jeshi la Magereza, Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza mchezo huo ulienda sare ya 0-0 huku Simba SC akitawala zaidi mchezo huo kwa muda mwingi kutokana na Kikosi bora cha timu yao licha ya ubora wa ngome ya ulinzi ya Prisons.
Tanzania Prisons waliitangulia Simba SC katika dakika ya 56 ya kipindi cha pili kupitia kwa Mchezaji wake, Salum Kimenya aliyepachika bao safi la faulo iliyopigwa nje kidogo ya lango la Simba SC.
Simba SC walilisakama lango la Prisons dakika zote baada ya kuwa nyuma kwa bao 1-0, Simba SC iliwatoa Wachezaji wake Rally Bwalya, Perfect Chikwende, na Mzamiru nafasi zao kuchukuliwa na Clatous Chama, Bernard Morrison na John Bocco.
Dakika 90+1, Simba SC walisawazisha bao kupitia kwa Mshambuliaji Luis Miquissone baada ya msako mkali katika lango la Prisons.
Hata hivyo, Tanzania Prisons walimkosa Kiungo wao, Jumanne Elfadhili baada kuonyeshwa Kadi Nyekundu baada ya kucheza vibaya dhidi ya Kiungo wa Simba SC, Mzamiru Yassin.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...