Charles James, Michuzi TV

SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa kufuatia kifo cha Rais Dk John Magufuli Watanzania wanakazi ya kuhakikisha wanaendeleza yale ambayo Raisi Magufuli alikuwa akiyafanya.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo, Job Ndugai amesema Rais Magufuli alikua mjenga nchi hasa katika suala zima la miundombinu na  miradi mikubwa mingi kama elimu, afya na barabara nakusema kuwa  ameacha alama kwenye kila nyanja.

Amesema kuwa kazi zote alizokuwa akizifanya Raisi Magufuli na hotuba alizozitoa bungeni sambamba na utekelezaji wa ilani ya  chama cha mapinduzi ya mwaka 2020/25 zitasimamiwa na kutekelezwa.

Aidha ameagiza Wabunge wote waliokuwa kwenye  ziara ya kukagua miradi ya  maendeleo kwenye kamati zao warudi haraka na mpaka sasa wabunge wote wako njiani kurudi dodoma.

Sambamba na hayo amesema Rais alikuwa muhimili wa pili wa Bunge hivyo ni pigo kwa Bunge na amemuachia kazi kubwa Makamu wa Rais Mama Samia na viongozi wote na serikali kwa ujumla  huku akitoa pole kwa Mke wa Rais Magufuli, Mama Janeth Magufuli, Familia yake na watu wa Chato na kwa Watanzania wote.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...