Na Mwaandishi Wetu Mtwara

SHIRIKA la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC) limeanza utekelezaji wa awamu ya pili ya kusambaza gesi mkoani Mtwara na Lindi ambapo wateja 500 wanatarajia kuunganishwa na nishati  hiyo.

Mkurungezi wa Shirka hilo Dkt James Mataragio alisema hayo mwisho mwa wiki iliyopita wakati wa uzinduzi wa mradi wa matumizi ya gesi asilia kwenye magari (CNG) katika kiwanda cha Dangote mkonia hapa.

“Katika mikoa ambayo tumekuwa tukifanya kazi ni pamoja na mtwara, mtwara tumejenga miundombinu ambayo ina uwezo wa kuunganisha wateja zaid ya 5000. Tuna mitambo ya zaidi ya kilomte 20 ambayo mpaka sasa hivi ninavyosema kuna awamu mbalimbali za uunganishaji wa gesi zinafanyika,” alisema.

Alisema katika mkoa wa Mtwara wateja 300 wanatarajiwa kuunganishwa na mkoa wa Lindi wateja 200 na baadae mkoa unaofuata utakuwa Pwani.

Katika hatua nyingine alisema kuwa kuna mradi mwingine unaendelea ya kuunganisha viwanda zaidi ya kumi mkoani Pwani ambapo mpka sasa viwanda 4 vimeshaunganishwa na vingine 2 wamesaini mktaba tayari kwa kwa kuunganisha gesi kwenye viwanda hivyo.

Katika hatua nyingine, Dr Mataragio amesema shirika hilo linaendelea na kazi ya kusambaza gesi mkoa wa Dar es Salaam kwa taasis mbalimbali zikiwemo za serikali ikiwemo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na maeneo mengine.

“Kwa upande wa Dar es Salaam, nyumba 500 zimeunganishwa na kuna mradi ambao unaendelea sasa hivi ambao mheshimiwa waziri uliuzindua, unahusisha kuunganisha nyumba 500 na vilevile  majumba polisi barrack,” amesema.

Alisema TPDC kwa kuwezeshwa na wizara wamekuwa wakifanya kazi ya kusambaza gesi kulingana na maelekezo ambayo wanapewa na serikali.

Vilevile Dkt Mataragio ameshukuru uongozi wa kiwanda cha Dangote Mtwara kwa kuwa mteja mkubwa wa TPDC kwenye masuala ya nishati hususan gesi ambapo alisema Dangote ni mteja wa pili baada ya shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuchukua ‘volume’ kubwa ya gesi.

Lakini kikubwa niongelee tukio la leo, tukio la leo kwetu ni tukio ambalo ni muhimu sana kwa sababu Dangote amekuwa ni mteja wetu mkuwa sana, Dangote alianza kutumia gesi kuanzia 2017, na mpka leo anatumia futi za ujazo milioni 20, ni kiwango kikubwa sana na tunawashukuru Dangote kuendelea kuonyesha njia,” alisema.

Alisema mwakani TPDC wanategemea kuwa na vituo vitano maeneo mbalimbali Dar es Salaam kwa ajili ya kusindika gesi kwenye magari

“Sisi nia yetu ni kwamba tutaongeza wigo na tutaongeza vituo ili wananchi wengi sana waweze kutumia CNG na mheshimiwa Mkuu wa Mtwara, Mtwara itakuwa ni moja kati ya mikoa ambayo tutaingalia kuweka kituo kidogo cha CNG ili wananch wa mtwara waweze kufaidika nah hii nishati mbadla ambayo ni rafiki kwa mazingira na bei nafuu,” alisema.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...