Na Mwandishi wetu, Chato
WACHIMBAJI
madini nchini wote kwa umoja wao kesho Ijumaa Machi 26 wakati jeneza
lenye mwili wa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt John Joseph Pombe
Magufuli utakaposhushwa rasmi kaburini wanapaswa kusimama walipo kwa
muda wa dakika tano.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) Lister Festo
Balegele amesema wachimbaji wote wa madini nchini wanapaswa kufanya
hivyo ili kutoa heshima zao za mwisho popote walipo.
"Tunapaswa
kufanya hivyo kutokana na msiba mkubwa uliolikumba Taifa la kuondolewa
na kipenzi chetu wachimbaji wadogo kwani alitupigania kwa nguvu zake
zote," amesema Balegele.
Amesema
ule muda utakaotangazwa wa kushusha rasmi jeneza la marehemu hayati
Dokta Magufuli kwenda kaburini inatakiwa wachimbaji wote wasimame walipo
kwa muda wa dakika tano ili kumuenzi.
"Kila
mmoja atakapokuwa hata kama upo mgodini tunaomba usimame pembeni kwa
dakika tano tuu ili kutoa heshima za mwisho kisha uendeleee na shughuli
yako," amesema Balegele.
Rais wa FEMATA John Bina (kushoto) na Katibu wa FEMATA
Lister Festo Balegele wakiwa Wilayani Chato Mkoani Geita, kwenye msiba
wa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt John Magufuli.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...