Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Baadhi
ya wananchi mkoani Pwani ,wamesema kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ,hayat dkt.John Magufuli kimewaacha midomo wazi
,na kudai watamkumbuka zaidi kwa kuwaachia miradi mikubwa ya kimkakati
ikiwemo kupanuliwa kwa barabara kuu ya Morogoro na mradi mkubwa wa umeme
wa Rufiji STIGO.
Aidha
wamemtakia mema makamu wa Rais Samia Suluhu safari yake ya kuongoza
nchi kuendeleza alipopaacha dkt.Magufuli na kumtakia kwenda na kasi
waliyoianza pamoja katika awamu ya tano .
Sophia Daniel,Makelele na Muhammad Patrick walisema kuondokewa na Magufuli wamepigwa butwaa kwani ni kifo cha ghafla.
Makelele
alifafanua, hayat Magufuli ameondoka Taifa likiwa bado linahitaji
uongozi wake uliojaa uadilifu na kupigania na kutetea wanyonge wakiwemo
wafanyabiashara ndogondogo ,madereva boda ,kundi la vijana wanawake na
wazee na walemavu.
"Nilishindwa
kujivumilia usiku niliposikia taarifa kutoka kwa makamu wa Rais kupitia
TBC ,nilistukia naangua kilio,huyu baba kama hujaguswa na msiba wake
utakuwa na matatizo" alisema Makelele.
Kwa
upande wake mkazi wa Mlandizi,Muhammad alisema mkoa wa Pwani umebaki na
kovu ,na wanakumbuka mengi yaliyofanywa kimkoa katika miradi mikubwa ya
kimkakati.
Magufuli
alitekeleza mengi kimkoa ikiwemo mradi wa reli ya kisasa SGR ni Mradi
unakwenda kufungua fursa za kiuchumi kwani umepita ndani ya Mkoa huo kwa
asilimia 60.
"Faida
nyingine tunayoenda kuipata kwa nguvu zake na uongozi wake ni gati la
Nyamisati,meli ya Mafia ,SGR, ,elimu bure,vituo vya Afya ,Maji Kisarawe
,Barabara ya Makurunge - Pangani ,Ukarabari wa Shule kongwe
,Umeme Vijijini serikali imetumia mamilioni ya fedha kuwezesha Vijiji
253 kupata Umeme.
Mwenyekiti wa UWT Kibaha Mjini Elina Mgonja ,alimlilia Dkt.Magufuli na kusema wana CCM kijumla na UWT wamepata pigo kubwa .
Alisema
kifo ni kazi ya mungu lakini wataendelea kukumbuka mazuri ambayo ni
mengi aliyoyafanya dkt Magufuli katika uongozi wake .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...