Na Mwandishi wetu, Babati

ZAIDI ya wananchi 239,858 Mkoani Manyara, wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji kwenye vijiji 87 ambapo kumetengwa vituo vya umma 617 vya kuchotea maji.

Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa) Mkoani Manyara, mhandisi Wolta Kirita ameyasema hayo mjini Babati kwenye siku ya wadau wa maji.

Mhandisi Kirita amesema wananchi hao wa vijiji hivyo 87 watakaonufaika na huduma hizo za maji ni kutoka wilaya za Simanjiro, Kiteto, Mbulu Hanang' na Babati.

Amesema Ruwasa mkoani Manyara, kwa mwaka wa fedha wa 2021 wamepanga kukusanya na kutumia sh18 bilioni kwa ajili ya kujenga, kukarabati na kuongeza mitandao ya maji.

Amesema miongoni mwa vipaumbele vyao kwa mwaka 2021/2022 ni ujenzi wa miradi mipya ili akiba ya kutosha iliyo tayari kutekelezwa wakati wowote pindi fedha zikipatikana.

"Pia vipaumbele vingine ni kupeleka huduma ya maji katika vituo vya afya, zahanati, shule za msingi na sekondari ambazo hazina huduma ya maji," amesema mhandisi Kirita.

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti amewapongeza Ruwasa kwa namna wanavyotekeleza miradi mbalimbali ya maji kwa wananchi waliopo kwenye wilaya za eneo hilo.

Mkirikiti amesema hata hivyo wananchi wa mkoa huo wanapaswa kujenga miundombinu ya kuvuna maji kwenye maeneo wanayoishi na taasisi za Serikali pindi mvua zinaponyesha.

"Kuliko kulalamikia ukosefu wa maji ni bora kuyavuna pindi mvua zinaponyesha, kwa wale mliofika wilaya ya Newala Mkoani Mtwara mtaona kila nyumba ina miundombinu ya kuvuna maji tuige hayo mambo mazuri," amesema Mkirikiti 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul amesema bado wananchi wa mji wa Babati wanalalamikia bei kubwa ya maji kupitia ankara tofauti na miji mingine nchini.

Gekul amesema amekuwa akilielezea hilo kila wakati na hata Bawasa wanapopunguza kwa sh40 wananchi wanaona bado wanatozwa bei ghali tofauti na maeneo mengine nchini.
 
Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Mkoani Manyara, mhandisi Wolta Kirita akizungumza Mjini Babati, kwenye siku ya wadau wa maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...