Katika kuadhimisha
kusherehekea siku ya Wanawake Duniani 2021, wasanii mbalimbali wa muziki wa
kizazi kipya hapa nchini wamekipongeza kinywaji cha Konyagi kwa kuwapa fursa ya
kuthamini ujasiri, ushupavu na uthubutu wa wanawake ambao wamejitoa katika
mafanikio ya kazi zao za kimuziki na kuwajenga katika Maisha kiujumla.
Mmoja wa wasanii hao, John
Simon Mseke, au maarufu kama Joh Makini, ‘Mwamba wa Kaskazini’, ameishukuru
Konyagi kwa fursa iliyompa ya kumzungumzia mwanamke ambaye anaamini amekuwa na
mchango mkubwa katika maisha yake na amesema mama yake mzazi ndio kila kitu
kwake na anabaki kuwa mwanamke wa nguvu katika maisha yake.
Joh Makini, mzaliwa wa
jijini Arusha, ambaye anajulikana kwa wimbo kama "Popote Chochote"
anasema mama yake amekuwa ndio kioo chake tangu akiwa mtoto mpaka sasa akiwa
mwanamuziki maarufu.
‘Siwezi kumaliza maneno
nikiamua kumzungumzia mama huyu shupavu,” Amesema Joh. “Mimi mwenyewe ni mzazi pia,
hivyo najua changamoto alizopitia mama yangu wakati nikiwa tumboni, aliponizaa
na wakati akinilea.” anasema mkali huyo ambaye pia ni mwanachama hai wa kundi
la "Weusi" kutoka Arusha.
Naye Juma Jux, maarufu kama
‘African Boy’ ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaosemekana kulipwa hela nyingi
katika show zake,amesema mama yake amekuwa na mchango mkubwa katika safari yake
ya kimuziki iliyokuwa na vikwazo vingi vya kukatisha tamaa.
Jux, anayeshirikiana na
wanamuziki mbalimbali katika nyimbo zake akiwemo Diamond Platnumz aliyeshirikiana
naye katika wimbo unaoitwa ‘Sugua” na ule wa ‘Juu’ alioshirikiana na mpenzi
wake wa zamani, Vanessa Mdee, anasema kuna watu wake kadhaa wa karibu, wakiwemo
wa familia yake waliomkatisha tama wakati anaanza muziki, lakini mama yake
alimwambia anaweza.
“Mama alinifundisha maisha,
namna ya kuwajali wanawake wengine na watu wote wanaonizunguka. Licha ya kuwa
peke yake, alinipa malezi bora na kunilea,” anaongeza Jux.
“Kwangu mimi, mama yangu ni
jasiri ‘ hero’ na kupitia siku hii muhimu, nawatakia wanawake wote heri ya
kusherehekea sikukuu ya wanawake Duniani” alimalizia kusema Jux huku akishukuru
Konyagi kwa kumpa fursa ya kutambua mchango wa mwanamke huyo muhimu kwake
maishani.
Siku ya Wanawake Duniani
imegusa kila mtu duniani kutokana na mchango wa akina mama, sio tu katika
malezi na kujenga familia bora, bali pia kushiriki shughuli za kiuchumi katika
nyenzo na nyanza mbalimbali, ikiwemo kufanya shughuli ambazo zimekuwa
zikifanywa na wanaume kama vile udereva, ufundi na nyinginezo nyingi. Konyagi
pia imetoa chupa yenye nembo maalumu ya mwanamke aliyeinua mikono kama
kiashiria cha kutambua umuhimu wa mwanamke katika jamii.
Katika wasanii wengine
waliopata fursa ya kutambua Wanawake muhimu katika Maisha yao ni Msanii Mwasiti
ambaye amemtambua Angelique Kidjo kama mwanamke aliyempa ujasiri kwa kazi zake
za muziki na mchango katika jamii.
Msanii Snura Mushi pia
ametambua watu watatu ambao ni bibi yake, muigizaji Monalisa pamoja na muimbaji
wa muziki wa taarab Sabaha Salum.
Mtangazaji wa Clouds FM Mamy
Baby pia alimaliza kwa kumtambua DJ Fetty aliyekua akifanya kazi katika kituo
hicho kama mwanamke jasiri aliyempa confidence katika tansia ambayo inaongozwa
Zaidi na wanaume.
“DJ Fetty ni mfano wa wanawake
wengine, akiwa mpambanaji kimaisha na
mwenye mafanikio katika kazi yake iliyopelekea atengeze jina kupitia vipindi
mbalimbali kama vile ‘Jahazi’ na vinginevyo vingi.” anasema mtangazaji huyo.
Maelezo ya wasanii hawa yamepewa
nguvu na kampuni ya Tanzania Distilleries Limited , inayotengeneza kinywaji cha
Konyagi katika kutambua ujasiri, weledi, ushupavu na uthubutu wa mwanamke
katika kujiletea maendeleo kupitia shughuli anazofanya katika jamiii
inayomzunguka.
Meneja Chapa wa Konyagi
inayotengenezwa na kampuni ya Tanzania Distilleries Limited, Pamela Kikuli
amesema kinywaji hicho ni kile kile kwa ladha na ubora lakini ameona kuna
umuhimu wa kutambua umuhimu wa Wanawake kwa kuweka nembo maalum kwa kipindi
hiki maalum.
Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka. Siku hiyo ilianza kuadhimishwa tarehe 8 Machi 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kuridhia siku hii kutumika kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...