Na mwandishi wetu, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilifanya oparesheni maalum ya kuwasaka wezi wa Pikipiki na kufanikiwa kuwakamata wakiwa na pikipiki 16 zidhaniwazo kuwa za wizi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Ilala leo, Kamanda wa polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa kuanzia Februari 01,2021 hadi Frbruari 28, 2021 watuhumiwa waliokutwa pikipiki hizo ni Stephen Paul (38), Mkazi wa Ulongoni A, Salum Mustafa (28), Mkazi wa Kigogo 3, Nsajigwa Kaisi (25), Mkazi wa Mongo la Ndege A
Wtuhumiwa wengine saba Oparesheni hiyo ilifanyika baada ya kupokea taarifa toka kwa wahanga wa matukio hayo ambayo yalikithiri katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Aidha watuhumiwa hao wamekuwa wakiiba pikipiki katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuzipeleka kwa Madalali ili kuziuza sehemu mbalimbali. watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na pikipiki zifuatazo;
(i)MC 967CRT aina ya Boxer
(ii) MC 922CSL aina ya Boxer
(iii)MC 646 CMS aina ya Boxer
(iv)MC 900 CRC aina ya Boxer
(v)MC 218 CSP aina ya Boxer
(vi)MC 339 CRQ aina ya Boxer
(vii)MC 677CNQ aina ya Boxer
(viii)MC 804 CRU aina ya Boxer
(ix) MC 271 CPT aina ya Boxer
(x) MC 618 CRC aina ya Boxer
(xi) MC 885 CKB aina ya Boxer
(xii) MC 832 CQF aina ya TVS
(xiii) MC 634 CKA aina ya TVS
(xiv) MC 412 CKP aina ya TVS
(xv) MC 543 AWN aina ya Boxer
(xvi) MC 735 CMF aina ya Boxer.
Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es salaam linaendelea na oparesheni na misako dhidi ya wizi wa pikipiki, magari na wahalifu wa makosa mengine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...