Mkazi wa Mbezi Tangibovu Said Mbasha(24), na wenzake watatu , wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin kilo 30.

Wengine ni Joseph Dalidali(27) maarufu Kama Mbezi Tangibovu; Allu Murugwa( 24) mkazi wa Kijitonyama na Fatima Shomari(24).

Akiwasomea mashtaka yao, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakim Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya, alidai washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa yao, Machi 3, 2021 katika eneo la Kijitonyama Wilaya Kinondoni, washtakiwa kwa pamoja walijihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 30.6, wakati wakijua ni kosa kisheria.

Pia,  Dalidali na Shomari, wanadaiwa Machi 3, 2021 katika eneo la Kinondoni mtaa wa Kasaba , washtakiwa hao wanadiwa kukutwa na gramu 2.63 za bangi, wakati wakijua kufanya biashara hiyo ni kosa kisheria.

Upelelezi haujakamilika na Hakimu Isaya aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 24, 2021 itakapotajwa .

Washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...