Na Mwandishi wetu, Kiteto
WAKAZI
wawili wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Leshoni Moita na Muunjuri
Tepeno, wamehukumiwa kwenda jela miezi sita kila mmoja kwa kushindwa
kulipa shilingi laki tano ya dhamana baada ya mtuhumiwa wa kesi ya
rushwa Moita Tepeno kuruka dhamana.
Hukumu
hiyo imetolewa na Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Kiteto, Mossy
Sasi baada ya washtakiwa hao kushindwa kulipa faini ya shilingi laki
tano kila mmoja, baada ya kumdhamini mtuhumiwa Tepeno kisha akatoroka.
Hakimu
Sasi amesema washtakiwa hao walimdhamini Tepeno kwenye kesi ya jinai
namba 22/2020 iliyopo mahakamani ya kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu.
Amesema
Tepeno alijipatia fedha hizo kwa udanganyifu kuwa ametumwa na Mkuu wa
Wilaya ya Kiteto Kanali Patrick Songea ili mtu ambaye binti yake
mwanafunzi alipata ujauzito asichukuliwe hatua.
Amesema
baada ya Tepeno kuruka dhamana mahakama iliamuru wadhamini wakamatwe na
kutakiwa kutoa fungu la dhamana sh500,000 kila mmoja na kukamatwa Machi
10 mwaka huu wakashindwa kulipa kisha wakapelekwa mahabusu.
Washtakiwa
hao walirudishwa tena mahakamani Machi 16 na kutakiwa kulipa fedha za
dhamana kila mmoja shilingi laki tano wakashindwa, ndipo wakahukumiwa
kwenda jela miezi kila mmoja na kisha wakapelekwa gereza la wilaya ya
Kiteto kuanza kifungo.
Mkuu
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Manyara,
Holle Joseph Makungu ametoa onyo kali kwa wana Manyara wote wenye mtindo
wa kuwadhamini washtakiwa mahakamani na kisha kuwatorosha waache mara
moja.
Makungu amesema kwa
watakaoshupaza shingo zao wafahamu kwamba yatawapata kama yaliyowapata
Tepeno na Leshoni kwani sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu, akizungumza na waandishi wa habari
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...