Mkutano
wa Kawaida wa 20 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya ngazi ya
Mawaziri uliofanyika leo katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki jijini Arusha, Tanzania; umekubaliana na kuahidi kuendelea
kushirikiana katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili
sekta ya afya katika Jumuiya.
Mkutano
huu uliotimishwa leo tarehe 23 Aprili 2021, umefanyika kwa siku tano
kuanzia tarehe 19 hadi 23 Aprili 2021, ulikuwa na lengo la kufanya
mapitio ya hatua ya maendeleo iliyofikiwa katika utekelezaji wa maamuzi
na maagizo yaliyotolewa na Mkutano uliopita wa Baraza la Mawaziri wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki na la Kisekta, sambamba na kuibua maeneo
mapya yanayohitajika kupewa kipaumbele kulingana na mapendekezo
yaliyotolewa na Kamati za Wataalamu.
Mkutano
huu uliokuwa ukiongozwa na Mhe. Mutahi Kagwe Waziri wa Afya wa Kenya
ambale pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, pamoja na masuala mengine
umepitia kujadili na kutoa maelekezo katika kutatua changamoto
mbalimbali, zinazokwamisha utekelezaji wa mikakati ya pamoja ya
kukabiliana na Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu unaosababishwa na Virusi
vya Korona (UVIKO-19), na usalama wa dawa na chakula katika Jumuiya.
Kila
Nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa nyakati tofauti
katika mkutano huo imeeleza utayari wake wa kushiriki kikamilifu katika
utekelezaji wa mikakati na mipango mbalimbali waliyokubaliana kuitumia
katika kutatua changamoto za sekta ya afya.
Mkutano
huu umehudhuriwa na Mawaziri kutoka Nchi zote Wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki wanaosimamia masuala ya Afya. Tanzania imewakilishwa na
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy
O. Gwajima (Mb)
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayesimamia Sekta za Uzalishaji na Jamii Mhe. Christophe Bazivamo (kulia) na Kaimu Mkuu wa Idara ya Afya, Sekretarieti ya Jumuiya Dkt. Michael Katende wakiratibu Mkutano wa 20 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya. |
Mkutano wa 20 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya ukiendelea jijini Arusha Tanzania |
Mkutano wa 20 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya ukiendelea jijini Arusha Tanzania |
Washiriki wa Mkutano wa 20 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja. |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...