Charles James, Michuzi TV
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amelihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kuwa Rais Machi 19 mwaka huu kufuatia kifo cha aliyekua Rais Dk John Magufuli ambapo ameahidi kulinda Demokrasia na Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Rais Samia amesema katika kulinda huko Demokrasia amepanga kukutana na viongozi wa vyama vya siasa ili kuona namna iliyo bora ya kufanya shughuli zao za kisiasa huku pia akiwataka watanzania kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria za Nchi.
Amesema katika hilo pia ameiomba Mahakama kupitia Jaji Mkuu kuhukumu yaliyo ya haki kwa wananchi na siyo kutoa hukumu zisizo kuwa na haki na zenye kuwaumiza Wananchi.
Rais Samia pia amezungumzia uwajibikaji kwa watumishi wa umma kwa kuendeleza nidhamu kwa watumishi wote na viongozi wake huku akisema serikali itakuja na mfumo mpya wa kupima mienendo na utendaji kazi wa viongozi wake.
" Pamoja na kusimamia utendaji kazi kwa watumishi wetu lakini pia tumepanga kutoa motisha kwa watumishi wetu kwa kupandisha madaraja na mishahara," Amesema Rais Samia.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...