Na Avila Kakingo-Michuzi Blog


UKISIKIA rangi ya Mamlaka nadhani utakumbuka kuwa ni Rangi Nyekundu ambayo hata mawaziri na Manaibu waziri na wabunge na wageni waalikwa walikatazwa kuvaa wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani alipoenda kuhutubia bunge Aprili 22, 2021.

Hii ilikuwa tofauti kwa leo katika Tuzo za Malkia wa nguvu 2021 zinazotolewa na Clouds Media Group katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyeyere kilichopo katika jiji la Ilala Mkoa wa Dar Es Salaam.

Kiukweli shughuli ilipambwa zaidi na Rangi Nyekundu na Nyeusi basi shughuli ilitaradadi na rangi zenye Mamlaka kihivyo achana na mitindo ya mishono ya wanawake kwa wanaume.

Yote kwa yote wanaume nao hawakuwa mbali kuwaunga mkono wanawake sio k we a kuja tuu katika shughuli ya Malkia wa Nguvu bali wengine walikwenda mbali zaidi kwa kuvaa nguo za kike kama Sketi, Mashati ya kitenge pamoja na kujitanda mitandio ambayo ukiangalia tuu unajua hapa ni mpokezano wa mume na mke au rafiki na rafikia yake ili kuhakikisha shughuli hiyo inakwenda sawia.

Bila shaka wale waliovaa nguo za Kawaida hawakukosa kupendezesha shughuli ya Malkia wa Nguvu kwa 2021.

Malkia wa nguvu 2021 ingia ulingoni hiyo ndio kauli mbiu iliyotaradadi kwa mwaka huu katika tuzo zilizoandaliwa na Clouds Media Group.






 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...