AKIWA na changamoto ya kutoona Afraaz Adam Mulji mtunzi na mpigaji mzuri wa piano ameendelea kuwa balozi wa maadili ulimwenguni kupitia sanaa yake ya muziki ambayo amekuwa akiitumia katika kuburudisha, kuonya na kueneza utamaduni wa Afrika.
Kupitia kipaji hicho kesho Aprili 22 Mulji anawaalika wadau wa sanaa kushuhudia kipaji chake katika kituo cha utamaduni cha Urusi 'The Russian Cultural Center' MKoani Dar es Salaam.
Mulji mzaliwa wa Tanzania na amekuwa akitumia mbinu mbalimbali za utunzi kupitia mafunzo ya muziki wa asili ya ukanda wa Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.
Licha ya kuwa na changamoto ya kuona bado anafanya vyema katika tasnia ya muziki katika karne ya 21 ambapo amekuwa mdadisi na mwenye kushirikiana na watu katika kupeleka muziki mbele zaidi pamoja na kujipatia riziki.
KATIKA TAMASHA HILO HAKUNA KIINGILIO,NI BURE.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...