Aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha siku tatu kinachofanyika Jijini Arusha kilichoshirikisha wataalam mbalimbali, mashirika binafsi na wadau wa Afya nchini.
"Tanzania tuko salama na wananchi wetu waendelee na maisha kama kawaida" alisema Dr. Subi.
Vilevile Dr. Subi amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote za ugonjwa wa Corona ikiwemo utamaduni wa kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni, kuvaa barakoa kwa usahihi na kuepuka misongamano isiyo ya lazima.
Aidha Dr. Subi ametoa wito wa kuendelea kuyalinda makundi ya watu walio katika hatari ya kuathiriwa zaidi na ugonjwa wa Corona ikiwa ni makundi ya wazee pamoja na watu wenye magonjwa sugu kama Kisukari na presha.
Zaidi Dr. Subi ameweka msisitizo kwa watanzania kuzingatia mtindo bora wa maisha ikiwa ni pamoja na kuzingatia mazoezi ya mwili na viungo na kuzingatia lishe bora ili kuongeza kinga za mwili katika kupambana maradhi ya kuambukiza pamoja na yale yasiyoambukiza.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...