Na Emmanuel J. Shilatu
Iyena!
Iyena! Wajumbe mkutano mkuu maalum wa Chama Cha Mapinduzi Taifa
nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Natumai
mmeitikia "kazi iendelee".
Tarehe
30/04/2021 mnaandika historia mpya nchini, Afrika na Dunia kwa kwenda
kumchagua Mwenyekiti CCM Taifa Mwanamke wa kwanza kabisa ambaye pia ni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
kuiongoza Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa katika historia yote ya maisha
yake tangu kizaliwa mwaka 1977. Ikumbukwe CCM ni chama cha kwanza
Afrika na cha pili Duniani kwa ukubwa, ukongwe na kushikiria madaraka
kwa muda mrefu, Wajumbe mkaongeze rekodi nyingine ya kumfanya Ndugu
Samia kuwa Mwanamke wa kwanza kuwa Mwenyekiti CCM Taifa.
Si
suala geni Mwanamke kuaminiwa ndani ya chama, walikuwepo akina Hayati
Bibi Titi Mohamed ambao walionyesha uwezo wa hali ya juu ndani ya chama
na kupitia jumuiya ya Wanawake (UWT), leo hii hatupaswi kuwa na hofu na
mashaka na Ndugu Samia Suluhu Hassan kiutendaji, tumpe nafasi ataivusha
salama CCM.
Wajumbe,
Ndugu Samia kwa muda mrefu maisha yake ameishi CCM, amekitumikia CCM
hivyo anaijua CCM kiunaga ubaga. Ndugu Samia ni mwana CCM kindaki ndaki
si wa kuoteshwa na hajawahi kuyumba, hakuna mwenye mashaka na uanachama
wake na uwezo wake pia.
Ndugu
Samia ana uzoefu wa muda mrefu kiutendaji ndani ya chama na serikalini.
CCM inakwenda kumpata Mwenyekiti jasiri, hodari, imara, Mzalendo,
Mchapa kazi kwa mujibu wa historia yake ndani ya chama na Serikalini.
Kama ni pishi basi limekwiva kweli kweli.
Nasikia
vikao vya Kamati KUU CCM Taifa, Halmashauri KUU CCM Taifa vimeruka
mtego wa wasioitakia mema CCM kwa kumpitisha kwa asilimia 100 kwa 100
kwa mapendekezo Ndugu Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti CCM Taifa na
sasa Wajumbe mkutano mkuu mkamalizie kazi kubwa iliyokwisha anzwa na
mkaidhihirishie Dunia kuwa CCM imejaa umoja, ushirikiano, upendo na
inayoendeshwa kwa mujibu wa vikao na Katiba na si maneno ya barabarani.
Wajumbe
msilegeze kamba, wembe ni ule ule kumkabidhi Ndugu Samia Suluhu Hassan
Uenyekiti CCM TAIFA ambao ni ndugu mmoja na Urais. Ngumu kutenganisha
kofia hizi kwa Mtu mmoja. Namwombea kura za ndiyo Ndugu Samia Suluhu
Hassan awe Mwenyekiti CCM Taifa
*Shilatu, E.J*
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...