Na Richard Mwamakafu - WHUSM, Dar es Salaam
Waziri
wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ametoa
pongezi kwa Tume ya Ushindani nchini (FCC) na Timu ya Soka ya Simba SC
kwa kumaliza mgogoro wao na kusisitiza vilabu vingine vya soka kuiga
mfano huo ili kuleta maendeleo ya mchezo wa soka nchini.
Mhe.Bashungwa
ametoa pongezi hizo leo Aprili 24, 2021 alipotembelea Mradi wa Ujenzi
wa Kituo cha michezo cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF)
kilichopo Kigamboni, Dar es Salaam
"Navikaribisha Vilabu vingine
kushirikiana na Serikali ili kuendana na Dira ya Serikali na
maelekezo ya Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutaka Sekta hii
kutoa ajira kubwa sana kwa vijana na kuchangia kwenye pato la nchi"
Mhe.Bashungwa
ametumia nafasi hiyo pia kuipongeza timu ya Simba kwa kufika hatua ya
robo fainali katika Michuano ya Klabu Bingwa Afrika, huku akiwasihi
Watanzania kuonyesha uzalendo wa kuiunga mkono timu hiyo
inayoitangaza nchi ya Tanzania kimataifa na kupitia kauli mbiu ya timu
hiyo ya (Visit Tanzania) "Tembelea Tanzania" katika Jezi zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...