Afisa Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Englibert Barnabas (kulia), akitoa ufafanuzi wa huduma zitolewazo na BRELA kwa mteja kutoka Kampuni ya Agrovision Limited Bw. Arfaan Ahmed Alwani, alipotembelea banda la BRELA, katika maonesho ya wadau wa Sekta ya Ujenzi, yanayofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Afisa Leseni  wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bi. Saada Kilabula ( aliyesimama kushoto) akitoa maelekezo ya huduma zitolewazo na BRELA kwa Msanifu majengo Bw. E.Nnunduma,  katika maonesho ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi, yanayofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, tarehe 27 -28 Mei, 2021.



Maafisa wa BRELA wakitoa elimu na huduma kwa watembeleaji wa Maonesho ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi yanayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mhandisi Leonard Chamuhiro, akipatiwa maelezo na maafisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), alipotembelea banda hilo mapema leo, baada ya ufunguzi wa maonesho ya Wadau  wa Sekta ya Ujenzi, yanayofanyika leo na kesho  katika viwanja vya Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Maafisa wa BRELA kutoka kushoto ni Afisa Usajili Bw. Englibert Barnabas, Msaidizi wa Usajili Bi. Yvonne Massele na Afisa Leseni Bi. Saada Kilabula.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...