Rais wa TFF Wallace Karia  na Afisa Mtendaji Mkuu Azam Media Limited Tido Mhando wakitia saini mkataba wa Haki za Televisheni Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Hoteli ya Hyatt Regencyc, Dar Es Salaam , wengine katika picha Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred (wa pili kutoka kushoto), Afisa Muendeshaji Azam Media Yahaya Mohamed (wa pili kutoka kulia), Mwanasheria wa TFF Rahim Shaban (wa kwanza kushoto) na Mwanasheria wa Azam Media Shani Christoms (wa kwanza kulia), mkataba huo wa miaka 10 una thamani ya bilioni 225.6
Rais wa TFF Wallace Karia  na Afisa Mtendaji Mkuu Azam Media Limited Tido Mhando wakibadilishana mkataba wa Haki za Televisheni Ligi Kuu ya Vodacom uliosainiwa kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Dar Es Salaam, mkataba huo wa miaka 10 una thamani ya bilioni 225.6

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania TFF limeingia mkataba na Kampuni ya Azam Media wa haki ya matangazo ya urushaji wa michezo ya Ligi kuu wenye thamani ya bilioni 225.6 za kitanzania kwa muda wa miaka 10.

Mkataba huo utakaoanza kwa msimu wa mwaka 2021 hadi 2031 umesainiwa na Mtendaji Mkuu wa Azam Media na Rais wa TFF Walace Karia na kushuhudiwa na wawakilishi wa klabu za Ligi Kuu, viongozi wa TFF na wadau wa mpira nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati waw hafla hiyo ua utiaji saini Karia amesema walitangaza zabuni hiyo Aprili mwaka huu na walianza mchakato huo wa kumpata mshindi mmoja kwa ajili ya kuonesha ligi kuu Tanzania bara.

Karia amesema, mbali na hilo klabu zitakazonufaika na udhamini huo zitatakiwa kurejesha mapato na matumizi kwa Shirikisho ili kupata mgao unaofuata na atakayeshindwa kutimiza basi atakuwa amejitoa.

"Kuna mfumo unakuja wa kupatiwa fedha na ziatolewa kwa njia ya kieletroniki tofauti na awali na kila klabu itatakiwa kuwasilisha mapato na matumizi ya kila mwezi ili kupata mgao unaofuata na atakayeshindwa kuwasilisha atakuwa amejitoa." Amesema Karia.

Aidha, fedha hizo zitagaiwa kila mwezi na zitakuwa ni kwa ajili ya mishahara ya wachezaji, usafiri na gharama zingine lakini hazitahusisha usajili au ulipaji wa madeni ya wachezaji na kuwasihi kufuata kanuni na kabla ya ligi msimu ujao kuanza watapatiwa ili waweze kuzijua.

Mkurugenzi wa Uendeshaji Tido Mhando amewashukuru TFF kwa kuwa washindi wa kuweza kupata haki ya kurusha matangazo na leo hii wanatia saini tena mkataba mpya kwa muda wa miaka 10.

Mhando amesema, wamekuwa moja ya wadau wakubwa wa maendeleo ya mpira nchini kwa muda wa miaka minane toka walivyopatiwa urushaji wa haki ya matangazo na TFF na kuzidi kuona thamani ya Ligi Kuu inazidi kukua na kuongeza ushindani na kuifanya ligi ya Tanzania kuwa katika ligi bora tatu Afrika.

Amesema, katika fedha hizo asilimia 67 zitakuwa ni malipo kwa timu za ligi kuu

Na fedha hizo zitakuwa zinaongezeka katika kila msimu ndani ya miaka 10 ili kuhakikisha ligi inaimarika na kuwa na ushindani.

"Azam wameongeza thamani ya Ligi na bingwa atapata Bonus ya Milioni 500, mshindi wa pili akipata milioni 250, mshindi wa tatu milion 225 na wa nne atapata milioni 200 na zawadi zitaongezeka kila.mwaka na kila timu itapata bonus kulingana na nafasi iliyopo," amesema Mhando.

Ameongeza kuwa dhamira ya Azam ni kuona TFF, Bodi ya Ligi na wadau wengine ikiwemo Serikali ni kuona kila mmoja anazingatia kanuni za ligi kuu, ushirikiano wa serikali na vyombo vya habari vya ndani , kuepuka manadiliko yanayoweza kuchochewa kisiasa, kuimarisha usimamizi wa fedha kwa klabu na fedha zinatumika kwa malengo yaliyowekwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...