Na Said Mwishehe, Michuzi TV

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA)limetoa tamko kulaani vitendo vya kinyama na uadui dhidi ya Taifa la Palestina na kuuwa rais wasio na hatia.

Akizungumza leo Mei 20,2021 jijini Dar es Salaam, Sheikh Mkuu na Muft wa Tanzania Abubakar Zubeir amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania linalaani vitendo vinavyoendelea Palestina na kwamba vitendo hivyo vinakwenda kinyume na misingi na haki za kibinadamu.

Ameongeza kuwa vitendo vinavyoendelea Palestina hivi sasa vinapingana na misingi ya dini kuu duniani ikiwemo dini ya Kiislamu, hivyo kwa tamko hilo BAKWATA linaitaka Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua stahiki kusitisha udhalimu huo usiokubalika.

"Aidha BAKWATA inawataka Waislamu wote Tanzania kuitumia Swala ya Ijumaa kusoma dua maalum kuliombea taifa la Palestina na kuendelea na dua za kunuti katika Swala zote tano kumuomba Mungu alinusuru Taifa hilo na ulimwengu kwa ujumla dhidi ya balaa hili kubwa na mabalaa mengine yote ulimwenguni,"amesema Muft wa Tanzania.

Akisoma tamko hilo ,amesema " Mwenyezi Mungu tunakuomba uufanye ulimwengu uione batili katika vazi lake la batili na uwaruzuku kuiepuka na utuoneshe haki katika vazo lake la haki na uturuzuku kuitafuta na kuitetea."

Sheikh Mkuu na Muft wa Tanzania Abubakar Zubeir(katikati) akitoa tamko la Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA)leo Mei 20,2021 jijini Dar es Salaam  kulaani vitendo vya mauaji vinavyoendelea katika Taifa la Palestina.Wengine alionao ni sehemu ya viongozi wa baraza hilo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...