WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa  amezisisitiza Taasisi za Media Council of Tanzania (MCT) pamoja na MISA TAN kutoa habari kwa jamii ambazo zinaleta matokeo chanya katika maendeleo ya nchi.


Mhe. Bashungwa ameyasema hayo Mei 27, 2021 Jijini Dodoma alipokutana na Viongozi wa Taasisi hizo ambapo amewaasa  kutanguliza uzalendo katika kutekeleza majukumu yao.

"Sio kila kitu ni kizuri kwa usalama wa nchi yetu ni vyema unapopata taarifa kabla ya kuichakata kuwa habari ipime kwanza kama ina maslahi ya Taifa, Endeleeni kutekeleza majukumu yenu na kushirikiana na Serikali"amesema Mhe.Bashungwa.

Akizungumza kwa niaba, Mwenyekiti wa MISA TAN Bi. Salome Kitomari  amemshukuru Waziri Bashungwa kwa kuwapa muda wakuonana nae ambapo  ameahidi kuendelea Kutoa Ushirikiano kwa serikali na Wizara kwa maendeleo ya Tasnia ya Habari Nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...