BENKI  ya NBC kupitia huduma yake ya #NBCShambani inayowalenga wateja wanaojishughulisha na kilimo imeongoza semina ya mafunzo kwa viongozi wa vyama zaidi ya 200 vya ushirika (AMCOS) Mkoani Tabora kwa lengo la kuwapa mafunzo mbalimbali.

Mafunzo hayo ni pamoja naumuhimu wa huduma za bima, matumizi ya fedha za kigeni  pamoja na elimu ya kuweka kumbukumbu za hesabu na matumizi sahihi ya mapato yao ili waweze kukopesheka kwa urahisi.


 Hafla hiyo ilifunguliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tabora, Bosco Ndunguru na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali akiwemo Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora, Absalom Cheliga na wakulima wa zao la tumbaku kutoka wilaya za Tabora Mjini, Sikonge na Uyui.


Pamoja na kuendesha mafunzo hayo Benki ya NBC kupitia Meneja wa Wateja Wadogo, Raymond Urassa walitoa zawadi ya pikipiki kwa Mwenyekiti wa Chama  Cha Msingi Solelansabo, Mary James Merrick ili kumsaidia katika shughuli za kuendesha chama na kuwatembelea wakulima. Pamoja na zawadi ya pikipiki hiyo, Benki ya NBC pia ilitoa baiskeli tatu kwa wakulima kutoka kwa vyama vya msingi mbali mbali kama pongezi kwa juhudi za kupata mazao mengikwa msimu uliopita.


Akifungua kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya,  Ndunguru aliipongeza Benki ya NBC kwa kuwawezesha na kuwapa mikopo na huduma za kibenki zenye gharama nafuu wakulima wa  zao la tumbaku ambalo kwa kiasi kikubwa linalochangia pato la mkoa huo. Aidha alitoa rai kwa benki hiyo kuingia kwenye mazao mengine ili kufungua fursa zaidi kwa wakulima wa mazao mengine. 


“Ni fursa kubwa sana kwa mkulima mmoja mmoja na ambao wako kwenye vyama mkoani kwetu kwa Benki ya NBC kuwa kwenye sekta ya kilimo na wakulima wanatakiwa kuichamgamki waanze kuzalisha kibiashara.” Alisema Ndunuru.


Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya NBC, Urassa alisema kwamba Benki ya NBC kupitia NBC Shambani imejipanga vizuri kuwahudumia wateja wake kupitia matawi yake nchi nzima wakulima wa mazao mbali mbali yakiwemo tumbaku, kahawa, parachichi, pamba na chai. 


Akiongelea huduma za kibenki kwa mkulima mmoja mmoja, Urassa alisema kuwa mkulima anaweza kufungua akaunti bila kuwa na kianzio na kuendesha akaunti bila kuwa na makato ya kila mwezi. “Pamoja na fursa ya akaunti za shilingi na dola, akaunti za vyama vya msingi pia hazina makato lakini pia zina gharama ndogo za uendeshaji kupeleka vyama vya msingi kuendesha shughuli zake kwa gharama nafuu na kuongeza ufanisi.” 


Kwa upande wake mnufaika wa zawadi ya pikipiki na Mwenyekiti wa Chama Cha Msingi Solelansabo, Mary James Merrick aliishukuru Benki ya NBC kwa zawadi hiyo na kusema kuwa itamsaidia katika kuendesha shuguli zake za chama kwa urahisi na ufanisi zaidi. Aidha alipongeza benki hiyo kwa kutoa huduma zilizo bora na mikopo yenye riba nafuu inayowawezesha wakulima kutimiza mahitaji yao ya pembejeo kwa wakati.


Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya NBC,  Raymond  Urassa akizungumza na viongozi wa vyama zaidi ya 200 vya ushirika (AMCOS) Mkoani Tabora wakati wa kongamani lilioandaliwa na benki hiyo lenye lengo la kuwapa mafunzo mbalimbali yakiwemo umuhimu wa huduma za bima, matumizi ya fedha za kigeni  pamoja na elimu ya kuweka kumbukumbu za hesabu na matumizi sahihi ya mapato yao ili waweze kukopesheka kwa urahisi. Hafla hiyoimefanyika mkoani humo jana  

Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru (watatukushoto)  akikabidhi pikipiki Mwenyekiti wa chama cha msingi  Solelansabo Mary James wakati wa kongamano lilioandaliwa na Benki ya NBC lenye lengo la kuwapa mafunzo wanachama na viongozi wa vyama mbali mbali vya ushirika Mkoani Tabora yakiwemo umuhimu wa huduma za bima, matumizi ya fedha za kigeni  pamoja na elimu ya kuweka kumbukumbu za hesabu na matumizi sahihi ya mapato yao ili waweze kukopesheka kwa urahisi wengine pichani ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya NBC,  Raymond  Urassa (wa pili kushoto) na Mrajis wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Tabora, Absalom Cheliga (kushoto) pamoja na viongozi wa chama cha msingi  Solelansabo.  Hafla hiyoimefanyika mkoani humo jana  






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...