Katibu
Mkuu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema
Serikali imejipanga kuisaidia Timu ya Taifa kwa kuipatia fedha ili
kuongeza ufanisi wa timu hiyo ndani na nje ya nchi.
Dkt.
Abbasi amesema hayo Mei 3, 2021 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es
salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Alfred Kidau ambapo wamezungumzia namna
ya kuiwezesha Timu ya Taifa (Taifa Stars) kwenye maandalizi ya michuano
ya awali ya kufunzu Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika mwezi Juni
hadi Agosti 2021.
“Ili kupata
matokeo mazuri wachezaji wetu lazima wawe vizuri kifedha hii itawasaidia
kisaikolojia kuweza kupata matokeo mazuri.” Alisema Dkt. Abbasi.
Ameongeza
kuwa Serikali imejipanga kuanzisha vyanzo mbalimbali vya mapato kwa
ajili ya michezo ikiwemo kurudisha mchezo wa Bahati Nasibu ((Sport
Betting Nationary Lottary).
Kwa
upande wake Bw. Alfread Kidau amesema maandalizi yote yamekamilika huku
akieleza kuwa changamoto iliyobaki ni ukosefu wa rasilimali fedha ambapo
ameshukuru namna Serikali inavyojipanga kukabili changamoto hiyo
ikiwemo kusaidia posho za wanamichezo kutolewa mapema.
Kikao hicho pia Kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania Bw. Yusuph Singo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...