Arum Mudgil mkurugenzi wa kampuni ya Tanwat akikata utepepamoja na baadhi yawatumishi wa hospital ya Tanwat ili kufungua na kuanza matumizi kwa wodi la akina mama lililofanyiwa ukarabati.
Edmund Mnubi meneja wa hospitali ya Tanwat akitoa ufafanuzi kwa mkurugenzi wa kampuni ya Tanwat namna ukarabati huo ulivyofanyika na ghalama zake ili kendelea kuboresha huduma za hospitali.

Baadhi ya vitanda na muonekano wa wodi ya akina mama mara baada ya kufanyiwa maboresho makubwa ndani ya hospital hiyo.


Na Amiri Kilagalila, Njombe

ILI kuongeza jitihada katika utoaji wa huduma za afya mjini Njombe,Hospitali ya Tanwat inayomilikiwa na kampuni ya Tanwat mkoani Njombe imefanya ukarabati wa zaidi ya Mil 15 katika wodi la wanawake kwa lengo la kuendelea kuthamini mchango wa wanawake katika jamii.

Akizungumza na vyombo vya habari, meneja wa hospital hiyo Edmund Mnubi amesema ukarabati huo umewapa kipaumbele akina mama kutokana na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na akina mama katika jamii.

‘Tumeanza kwa kuwapa kipumbele mama zetu kutokana na kuthamini mchango wao kwenye jamii na kwa ukarabti huu tunaamini watapata huduma ya matibabu katika sehemu inayoendanana hadhi zao kwa kuzingatia mazingira safi na salama’alisema Edmund Mnubi

Jackline Shaka ni miongoni mwa watumishikatika hospitali hiyo,amesema kuboreshwa kwa wodi hiyo ni mpango endelevu wak kuendelea kuboresha huduma ndani ya hospitali na wanaamini itasaidia kwa kiasi kikbuwa kuendelea kuvutia wateja.

‘Katika hospitali yetu tunajalisana afya kwa hiyo mtu anapokuja hapa kukiwa na mazingira safi tunaamini mteja wetu atajiskia vizuri Zaidi,awali muonekano katika wodi hii haukuwa hivi lakini maboresho yamekuwa makubwa zaidi’alisema Jackline Shaka

Benjamini Ngajiro ni mmoja wa wateja aliyefika katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu ,amepongeza huduma zinazotolewa katika hospital hiyo Pamoja na kushukuru uboreshwaji wa miundombinu na muonekano wa majengo katika hospiatal.

Arum Mudgil ni mkurugenzi wa kampuni ya Tanwat amewapongeza watumishi wa hospital hiyo huku akiahidi kuendelea kuboresha miundombinu.

‘Ninawapongeza watumishi wa hospital kwa kazi kubwa wanayoifanya kwasababu ninona kujitoa kwao kwa kiasi kikubwa kwa hiyo tutaendelea kushirikiana kwa karibu na niwakaribishe watu wote waendelee kufika katika hosptili hii’alisema Arum Mudgil


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...