Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Mchakato wa Kumpata Mrembo atakayewakilisha Mkoa wa Kagera katika Shindano la Miss Tanzania 2021, umeanza kushika Kasi katika Mkoa wa Kagera, Baada ya Kamati ya Maandalizi kwa kushirikiana na Waandaaji Kutambulisha Rasmi zawadi ya Mshindi wa Taji hilo.

Akitambulisha zawadi hiyo mratibu wa Shindano la Miss Kagera 2021 Regina Zachwa kutoka Zachwa Investment, amesema Mwaka huu wao Kama waandaaji waliopewa dhamana hiyo, kwa kushirikiana na Serengeti Breweries Ltd pamoja na Wadau wengine wameamua kuandaa zawadi ya Gari Mpya, aina ya  Rectus  yenye Thamani ya Shilingi Milioni 18          ambayo atapewa Mshindi wa Kwanza katika Shindano hilo.

"..Mara hii Miss Kagera itakuwa Kivingine na kubwa zaidi, ukizingatia Ukubwa wa zawadi ya Mshindi, lakini pia wapo Baadhi ya waheshimiwa wakiwemo Wabunge ambao wameamua kussuport Jambo Hili, hivyo tunategemea pia ushindani utakuwa Mkubwa Sana..." Amesema Regina.

Zawadi hiyo ya Gari imezinduliwa Rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe Deodatus Kinawiro katika Viwanja vya Makao Makuu ya Redio Kasibante FM inayomilikiwa na Zachwa Investment, ambaye kwa Upande wake amesema Shindano hilo litautangaza Mkoa wa Kagera katika nyanja tofauti zikiwemo za kiuchumi na kiutamaduni, na kuwataka wasichana kujitokeza kushiriki katika mchakato huo.

Pamoja na Mambo mengine Kamati hiyo ya Maandalizi ya Shindano la Miss Kagera, imeweka wazi ratiba ya Shindano hilo kwa Wilaya za Mkoa Kagera ambapo Mwezi huu, Tarehe 28 na 29 Shindano litaanzia Biharamulo na Ngara, Mwezi ujao itakuwa zamu ya Muleba na Missenyi, Mwezi wa Saba zamu ya Karagwe na Kyerwa na Kisha kilele cha Shindano ni Agosti 08,  2021 ndani ya Bukoba Manispaa.

 Mratibu wa Shindano la Miss Kagera Regina Zachwa akifurahi na Zawadi ya Mshindi Mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera kabla ya kutambulishwa kwa Wanahabari mapema Mei 26, 2021.


 Akinadada Mabalozi wa Miss Kagera wakisindikiza Gari la zawadi katika msafara wa Kuelekea Makao Makuu ya Redio Kasibante kwa ajili ya Utambulisho.


 Gari aina ya Rectus ambalo litashindaniwa  na Warembo kutoka Wilaya zinazounda Mkoa wa Kagera Kama linavyoonekana pichani.


 Meneja Vipindi wa Kasibante FM Ndg. Jerome John akifafanua namna wao Kama Redio walivyokuja na wazo la kuwa waandaaji wa Shindano la Miss Kagera 2021.
 Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe Deodatus Kinawiro akizungumza mbele ya Vyombo Vya Habari juu ya Umuhimu wa Shindano la Miss Kagera 2021, wakati wa Utambulisho wa Zawadi ya Mshindi wa kwanza kwa Mwaka huu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Zachwa Investment Bwana Muganyizi Zachwa, akitolea Ufafanuzi zawadi ya Gari ambapo amesema Mara hii hakuna janja janja



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...