Na Woinde Shizza, Michuzi Tv ARUMERU
Hali ya Taharuki imewakumba wananchi wa Vijiji vya Embaseni na Maji ya chai wilayani Arumeru Mkoani Hapa ,kufuatia mnyama aina ya kiboko kuvamia makazi yao na kuwajeruhi watu wawili na kujaribu pikipiki.Kiboko
huyo anayedaiwa kutoroka kutoka hifadhi ya Taifa ya Arusha ANAPA ,na
kuzua taharuki katika vijiji hivyo mapema jana majira ya asubuhi pale
alipoibuka ghafla na kushambulia wakazi wawili ambao hali zao
zitaendelea vizuri.
Kwa
mujibu wa mwenyekiti wa Kijiji cha Maji ya Chai ,David Mbise mnyama huyo
alionekana akizunguka katika Kijiji hicho Jana asubuhi hata hivyo watu
walianza kumzonga kwa kufuata nyuma kila napokwenda ndio alipopandwa na
hasira na kuwafukuza watu aliokutana nao mbele yake na kuwajeruhi
wawili.
"Wakati watu
wakimfuatilia ndipo alimkamata mtu mmoja na kumng'ata hadi kumvunja mguu
na mwingine alimng'ata mgongoni na baadaye aliikuta pikipiki yangu
imeengeshwa ambapo nayo aliing'ata na kuiharibu alisema shuhuda.
Naye
mwenyekiti wa Kijiji Cha Embaseni Joshua Nasari alisema kuwa Mara baada
ya mnyama kujeruhi watu katika Kijiji Cha Maji ya chai alikiambia na
kuvuka mto na kuingia katika Kijiji chake lakini hakuwez kujeruhi mtu
yeyote lakini Askari wa wanyama pori walifanikiwa kumuua .
Baadhi
ya wananchi wa vijiji hivyo walionufaika na Nyama ya Kiboko baada hiyo
,Daruweshi Abdala alisema kuwa hakuwahi kula nyama ya kiboko Ia ujio
wake kumesababisha kupata kitoweo ambacho hakukitarajia.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambaye Ni mwenyekiti
wa ulinzi na usalama wilaya ya Arumeru alithibitisha kujeruhiwa kwa watu
wawili akiwemo mmoja kuvunjwa mkuu.
Alisema
Mara baada ya kupata taarifa alifika eneo la tukio na kushuhudia
majeruhi hao huku majeruji mwingine akiwa amejeruhiwa eneo la ubavuni.
Hata
hivyo Muro aliwasihi wananchi hao kuchukua tahadhari kutokana na
wanyama hao kuvamia maeneo ya makazi kwa kutoa taarifa mapema kwa vyombo
husika ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.
Aidha
alizitaka mamlaka.husika ikiwemo hifadhi za Taifa Tanapa kuona umuhimu
wa kugharamia matibabu ya wahanga wa wanyama hao kwa haraka zaidi na
kuona namna ya haraka ya kuwalipa kifuta jasho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...