Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mko wa Njombe ni miongoni mwa mikoa ya Tanzania yenye changamoto kubwa ya tatizo la moto hususani kwenye majengo ya shule,hifadhi hata misitu kutoakana na shughuli mbali mbali zikiwemo za kilimo mkoani humo.

Kwa kuliona hilo wataalam mbali mbali wameendendelea kutoa elimu ya moto ili kudhibiti hasara kubwa ambazo zinaweza kujitokeza mara baada ya changamoto hiyo.Ahmed Rizvi ni mmoja wa wageni kutoka jijini Dar es Salaam na mtaalamu wa maswala ya moto amefika mkoani Njombe na kutoa elimu ya kudhibiti moto katika kijiji cha Vanilla ili kuweza kuokoa hasara za mabilioni ya fedha yanayoweza kupotea.

“Zao hili ni jipya bado hapa Tanzania na kuna ujenzi mkubwa wa hizi Green house unaendelea Njombe kwa ghalama kubwa sana na hapa nikiangalia kwenye shamba utaona zao linategemea sana na haya majani,kwa hiyo ukiangalia haya mazingira akipita mtu anayevuta sigara anaweza kuleta madhara ndio maana tumetoa elimu kwa hawa vijana wanaoendelea na shughuli za kilimo kwenye huu uwekezaji”alisema Ahmed Rizvi

Ali Jawad ni miongoni mwa wageni waliofika ili kujifunza uwekezaji katika zao la Vanilla mkoani Njombe kutokana na zao hilo lenye ghalama kubwa kuendelea kukuwa kwa kasi mkoani humo.Amesema licha ya kuwa na shughuli zao ikiwemo kumilika taasisi za mashindano ya magari pamoja na kusaidia jamii lakini wamekuwa wakijihusiha katika kilimo na ufugaji hapa nchini ndio maana wamevutiwa pia katika kilimo cha Vanilla kinachoendelea mkoani Njombe.

“Tumependezewa hapa na kijiji cha Vanilla kwa kuwa tunajua kidunia ni zao namba mbili yenye ghalama baada ya Zafloo,na leo tumefika hapa na kutoa mawezo yetu na sisi kama wadau tuweze kuwekeza na pia kuvutia wawekezaji wengine”alisema Ali Jawad

Aidha ametoa rai kwa watanzani kuweza kujitokeza zaidi na kuweza katika zao hilo lenye bei juu duniani na imekuwa na uhaba katika upatikanaji wake kwa kuwa 80% ya zao hilo duniani inapatikana katika nchi ya Madagascar pekee.

“Asilimia 80 ya Vanilla inatoka Madagascar sasa kama Madagascar wanaweza kufanya hivi kwanini Tanzania Tushindwe, wakati tuna sehemu za joto tuna sehemu za baridi na sisi tunaweza kulima zao hili na kuwafikia wenzetu”alisema tena Ali Jawad

Saimon Mkondya ni mkurugenzi wa kampuni ya Vanilla interneational inayojishughulisha na kilimo hicho katika mkoa wa Njombe ikiwemo kwenye kijiji kilichopewa jina la kijiji cha Vanilla kilichopo Idunda kata ya Yakobi.Ameshukuru watumishi wake kupata elimu ya kuepukana na majanga ya moto.

“Katika wageni wetu tuliowapokea tunashukuru pia tumempata mtaalamu wa kuzima moto,na ameweza kutufundisha jinsi ya kuepukana na majanga ya moto pamoja na kuzima katika hizi green house zetu,na ukizingatia zao hili ni ghali sana ambalo kilo moja inazidi milioni moja kwa hiyo moto ukitokea tutapata hasara ya mabilioni ya fedha”alisema Saimon Mkondya

Zaidi ya wageni 20 wamefika katika kijiji hicho cha Vanilla ili kujifunza namna kilimo hicho kinavyoendelea pamoja uwekezaji wake huku watumishi wa kijiji hicho 150 wakinufaika na elimu ya moto.


Ahmed Rizvi mmoja wa wageni kutoka jijini Dar es Salaam na mtaalamu wa maswala ya moto akieleza namna walivyotoa elimu ya moto kwenye kijiji cha vanilla kutokana na kuvutiwa na uwekezaji mkuwa uliofanyika kwenye kijiji hicho.

:Baadhi ya wafanyakazi wanaoendelea na shughuli za kilimo kwenye kijiji cha Vanilla wakisikiliza kwa makini elimu ya moto iliyokuwa inatolewa na mtaalamu mara baada ya kushuhudia uwekezaji mkuwa unaondelea Njombe.

Wageni wa mataifa mbali mbali wakizungumza na mmoja watumishi wa kijiji cha Vanilla mara baada ya kupendezewa na kilimo katika kata ya Yakobi mjini Njombe
 
Saimon Mkondya  mkurugenzi wa kampuni ya Vanilla international akieleza jinsi anavyofurahi kupokea wageni na kufikia uwekezaji wa kiwango cha juu katika zao hilo hapa Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...