Na Woinde Shizza ,michuzi Tv ARUSHA
WANANCHI wanapaswa kuanza kufanya kilimo na ufugaji wenye tija. Namna bora ya kukabiliana na changamoto za wafugaji na wakulima ni kutafuta mbinu shirikishi zitakazohusisha wadau katika utatuzi, ili kuendelea kuongeza uzalishaji. Wadau wa kilimo na ufugaji wanahitaji kuunganisha nguvu kwa pamoja badala ya kumuachia mkulima na mfugaji kuhangaika na utatuzi mwenyewe.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda katika ziara ya siku ya pili kutembelea wakulima na wafugaji katika kijiji cha Chemchem, kujionea miradi ya shirika lisilo la serikali la Food for his children linavyosaidia kuimarisha familia duni kuweza kujikwamua kiuchumi.

 Amepongeza jitihada zinazofanywa na shirika hilo kwa wananchi wa Karatu, hasa kwa mafanikio ya dhahiri yaliyojikita katika ufugaji wa mbuzi wa kisasa aina ya sane. Lakini kwa namna wananchi walivyopokea miradi hiyo na kuona kama ni miradi ambayo inagusa maisha yao.

amesema changamoto kubwa ya ufugaji wa kisasa ni malisho ya mifugo ambayo kama ikitatuliwa itamsaidia mfugaji kupata maziwa kwa wingi.

 Ametoa rai kwa shirika la Food for his children kuona namna ya kuja na mbinu shirikishi ili kumkwamua mfugaji hasa katika adha ya kupata malisho ya mifugo.

 Amesema kama mbuzi mmoja wa kisasa kwa makadirio ya juu akitunzwa vizuri anaweza kutoa lita tano kwa siku kwa maana ya kukamuliwa mara mbili asubuhi na jioni. Basi ipo haja ya shirika kukaa na wafugaji ili kuja na ufumbuzi wa changamoto zao kwa pamoja ili mwananchi aweze kunufaika zaidia na ufugaji.

Mh. Kayanda ameshauri shirika la Food for his children kupata takwimu sahihi za wananchi waliojihusisha na mradi huo. Amesema kupata takwimu za namna mbuzi wanavyozaliana lakini pia kupata takwimu za kiasi cha mbuzi waliouzwa.

 Amesema takwimu ndio ziatakazosaidia kujua mafanikio ya mradi na udhaifu wa mradi. Ameongeza kusema kuwa katika taarifa zao ni vyema wakawa na wasifu za mfugaji mmoja mmoja lengo likiwa ni kufahamu matokeo ya mradi kwa ujumla na matokeo ya mradi kwa mwananchi mmoja mmoja.

Meneja wa mradi Bi, Honorina Honorati amesema mbuzi wa kisasa wanaosambazwa na shirika la Food for his children, wanatabia ya kuzaa mapacha isipokuwa tu kwa uzazi wa kwanza. Ameongeza kusema mbuzi hao wanaweza kuzaa mara mbili kwa mwaka hivyo kumfanya mfugaji kuongeza idadi ya mbuzi lakini kufaidika na maziwa ya mbuzi.

Bi, Honorati amesema wafugaji wengi wa mbuzi wananufaika kwa biashara ya kuuza mabeberu ambao wanauza mpaka kiasi cha shilingi 200,000 kulingana na ukubwa na uzito. Amesema matarajio ya mradi ni kuona watu wengi wanafanikiwa, na wanapenda kujihusisha kaitika ufugaji wa mbuzi wa kisasa. Ili kutoa fursa kwa watu wengine wasioujua mradi kufundishwa na kuelewa misingi ya mradi.

Mama fabiola, Mfugaji wa mbuzi wa kisasa katika kijij cha Chemchem amesema kitu kinacholeta faraja katika mradi huo ni upatikanaji wa maziwa ambao unawawezesha kupata kipatao. Amesema katika miradi yake ya ujenzi hutegemea kuuza mabeberu ambao wamekuwa na soko kubwa. Amesema katika kijiji Chemchem changamoto kubwa wanayopata wafugaji ni fisi ambao wananyemelea mifugo yao wakati wa usiku.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Abbas Kayanda akiangalia mmoja wa mbuzi wakati wa alipofanya ziara ya kutembelea wakulima na wafugaji katika kijiji cha Chemchem, kujionea miradi ya shirika lisilo la serikali la Food for his children linavyosaidia kuimarisha familia duni kuweza kujikwamua kiuchumi.
(Picha na Woinde Shizza , ARUSHA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...