Khadija Seif, Michuzi Tv

WABUNIFU wa mavazi sita wamehitimu darasa la ubunifu wa mavazi 101 lililokua limeandaliwa na mbunifu mkongwe wa mavazi nchini, Ally Remtulah lengo likiwa kuwajengea uwezo wabunifu wachanga.

Akizungumza wakati wa jukwaa kuhitimisha awamu ya kwanza ya mafunzo ya ubunifu lililoandaliwa katika ukumbi wa The Drum Mkoani Dar es salaam, Remtulah amesema  kutokana na kupenda kwake kuona Tanzania inakua na wabunifu wengi watakaoweza kushindana katika soko la kimataifa ameamua kuwainua wabunifu chipukizi ka kuendesha darasa ambalo linalenga kuwaimarisha wabunifu hao pamoja na kuwatambulisha kwenye Sekta ya ubunifu wa Mavazi.

Amesema darasa hilo la ubunifu wa mavazi linachukua muda wa miezi mitatu huku likiwakutanisha wabunifu wachanga na wakongwe ili waweze kuongezewa ubora wa kushindana katika soko la kukuza tasnia hiyo ya ubunifu wa mavazi.

Akizungumzia uchache wa wabunifu waliohudhuria darasa hilo, Remtulah amesema changamoto ipo kwenye fedha ya kuendesha madarasa hayo na ndio maana ameanza na watu wachache kwanza.

"Kuna baadhi ya vitu vinakua vigumu kuwapatia wanafunzi hao kwa wakati kutokana na changamoto ya kifedha, hivyo naamini kadri muda utakavyokua unaendana tutajitahidi kumaliza changamoto zilizopo tuwe na wanafunzi wengi zaidi," Amesema Remtulah.

Amewapongza Baraza la Sanaa nchini (BASATA) Kwa kuendelea kutoa Ushirikiano kwa majukwaa ya Mavazi na kutoa ruhusa kuonyesha Mavazi mbalimbali.

"Mwanzo ilikua shida hasa kwa wabunifu kuonyesha au kupita jukwaa na mavazi kama ya usiku au ya ufukweni kutokana na mavazi hayo kuonekana ni nje ya maadili yetu lakini kutokana na walezi hao kukubaliana  na hilo imefanya hata wabunifu wetu kuongeza uwezo na jitihada za kutengeneza mavazi hayo," Amesema.


Kwa upande wake Mbunifu Anna Joseph ambae ni Miongoni mwa waliopatiwa Mafunzo hayo amesema darasa hilo limemfungulia milango mingi ikiwemo kujuana na watu wengi na kuongeza wigo wa kukuza kipaji chake.

"Imenijengea uwezo wa  vitu vingi hasa kujua misingi ya kufanya kazi kwa kuipenda na kwa kujitolea , kufanya kazi kwa kushirikiana Kama timu moja yenye malengo sawa lakini pia darasa hili limenikutanisha na watu wengi sana," Amesema Anna.

Mbunifu huyo amesema Remtulah ni Miongoni mwa vijana wenye uwezo na moyo wa kusaidia vijana wengine kujiendeleza na kuamini vipaji vya wengine.

" Kwa mara ya kwanza nimetambulisha vazi langu la ufukweni japo wakati warembo wanapita nalo jukwaani ilikua gumzo kutokana na jamii yetu bado haijazoea lakini tunashukuru BASATA wameturuhusu tuoneshe na wametuunga mkono," Amesema Anna.


Baadhi ya Warembo wakipita jukwaani kuonyesha Mavazi yaliyobuniwa na wanafunzi waliopatiwa Mafunzo Miezi 3 katika darasa la Mkongwe wa Ubunifu wa Mavazi Ally Remtulah katika ukumbi wa The Drum Masaki Dar es salaam.

 Mbunifu Mkongwe Ally Remtulah akizungumza Mara baada ya kutambulisha Wabunifu hao 6 katika awamu ya Kwanza ya Mafunzo hayo na kuwahaidi Wadau kuendelea na Awamu  ya pili ya Mafunzo hayo .

 Moja wabunifu waliopatiwa Mafunzo katika darasa la Ally Remtulah 101 akitambulisha Mavazi ambayo ameyabuni akiwa katika Mafunzo hayo

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...