Na Mwandishi Wetu , Zanzibar
KAMPUNI
ya Lavy Beauty Limited inayoongozwa na Mkurugenzi wake Flaviana
Matata imetoa taulo za kike kwa wasichana 270 ambao ni wanafunzi wa
Shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki iliyopo Maeneo ya Mazizini
Kisiwani Zanzibar.
Pia zawadi kama hizo zimetolewa na Lavy Jijini Dodoma kwa wasichana 480 ikiwa ni Katika kuadhimisha siku ya Hedhi Duniani.
Flaviana
alitoa zawadi hizo leo shuleni hapa aliongeza kwa kuwahi anaiomba
Serikali iwaondolee kodi kubwa ambayo wanalipa kwa sababu bidhaa ya
taulo hizo za kike ni bidhaa isiyokuwa na faida pia ni muhimu kwa
matumizi ya mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla.
Sisi tunaingia gharama katika kutengeneza taulo zenye ubora hivyo nashauri waweke mpango wa kuzinunua na kugawa bure mashuleni.
Meneja
wa Marie Stopped Zanzibar David Mbange aliongeza kwa kusema kuwa kuwa
siku ya hedhi duniani huadhimishwa kila ifikapo Mei 28 Mei kila mwaka
"Siku hii ina lengo la
kuwakutanisha wadau mbalimbali kwa dhumuni la kuongeza uelewa kuhusu masuala ya
hedhi na kuhamasisha upatikanaji maji safi , taulo(visodo) kwa wasichana na wanawake
hasa wale walio katika mazingira magumu.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kiembe Samaki Mussa Abdi Khamis amesema kuwa
amefurahishwa na ujio wa Lavy na kutoa zawadi kwa wanfunzi wote wa kike
na kiume.
Alisema
kuwa hii Elimu wazazi wengi hawana muda wa kuwaelewesha vijana wao kwa
uwazi huku akisisitiza kuwa mazingira ya hapa shuleni kwake ni mazuri
na rafiki kwani Kuna patikana maji pia wanna kisima na Kuna
waalimuwanaotoa ushauri nasaha.
Pia Lavy Limited Company tangu imeanzishwa inatoa taulo za kike kwa wasichana 2993 bure nchi nzima.
Zawadi hizo za vitaulo zimetolewa katika mikoa mbalimbali ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Hedhi Duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...