Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wa Kilabu ya Crystal Palace
inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) na Mchezaji wa timu ya taifa ya
Ufaransa amekubali ombi la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa Balozi wa
Hiari wa Utalii wa Tanzania. Mamadou amekubali ombi hili wakati
alipokutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Betrita Lyimo katika
Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.
Mamadou ambaye ni raia wa
Ufaransa amewasili nchini Tanzania tarehe 26/5/2021 kwa mapumziko ya
siku 10 akiwa ameambatana na familia yake wametembelea vivutio vya
utalii vya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Kijiji cha Wamasai cha Seneto,
Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro na Visiwa vya Zanzibar.
Aidha,
Timu ya Waandishi wa habari wa Televishen ya TF1 ya nchini Ufaransa
imewalisili nchini Tanzania tarehe 27/5/2021 kwa lengo la kutengeneza
makala maalumu ya ziara ya Mamadou itakayotumika kutangaza utalii wa
Tanzania kwenye soko la utalii la Ufaransa hususani maeneo yote ya
vivutio vya utalii aliyotembelea mchezaji huyu Maarufu.
Tanzania inaendelea inapokea wanamichezo kutoka nchi mbalimbali duniani
wanaokuja na familia zao kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania. Hii
ni fursa adhimu kwa TTB kuendelea kushirikiana na wanamichezo kutangaza
utalii wa Tanzania hasa wenye wafuasi wengi kwenye mitandao yao ya
kijamii ambayo ni nyenzo muhimu yenye kufikifiksha ujumbe kwa watu wengi
ndani ya muda mfupi. kwa ziara ya matembezi ya siku 10. Mchezaji huyu
Mchezaji
Mamadou Sakho na familia yake wakiangalia burudani ya ngoma ya Kimasai
wakati alipotembelea kijiji cha Wamasai wanaoishi katika Hifadhi ya
Bonde la Ngorongoro.
Mchezaji
mpira wa Miguu Mamadou Sakho na familia yake wakionyesha vyeti
walivyopata baada ya kumaliza safari yao ya utalii wa kutumia puto
(Balloon Safari) katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.
Mchezaji mpira wa Miguu Mamadou Sakho akiwa na familia yake katika hifadhi ya Bonde la Ngorongoro. 
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB) Betrita Lyimo akiwa pamoja na
Mamadou Sakho, Mchezaji wa mpira wa miguu kilabu ya Crystal Palace
inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) na mchezaji wa timu ya Taifa ya
Ufaransa.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...