Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang'ata ameishauri serikali kuharakisha malipo ya wakandarasi nchini ambao wanaidai serikali baada ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu nchini.
Pia Mbunge Mwakang'ata ameiomba serikali kuanza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga Mjini ambao umetelekezwa licha ya kulipa fidia walioupisha ujenzi. Aidha mbunge huyo ameiomba serikali kuijenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Kibaoni-Majimoto hadi Mlowo kutokana na umuhimu wake kiuchumi.
Mwakanga'ata alitoa ushauri huo alipokuwa akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakati wa Mkutano wa Tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kikao cha 30 jijini Dodoma Mei 18, 2021.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mbunge Mwakang'ata akitoa ushauri wake huo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...