Jane Edward Michuzi TV, Arusha
 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Godwin Mollely ametoa siku Tatu kuongezwa kwa vyumba vya kupimia Corona watalii Wanaoingia Nchini kupitia Uwanja wa kimataifa Kia mkoani Kilimanjaro.

Akizingumza mkoani Arusha mara baada ya kutembelea na kuona shughuli katika uwanja huo wa ndege Dr mollely ametoa maelekezo kwa Wataalamu wa Afya Wa mkoa wa Kilimanjaro kuongeza watumishi na vyumba vya kupimia ILi kutowachelewesha watalii na wageni Wanaoingia Nchini ILi kuendelea na safari za kutembelea hifadhi za Taifa bila kuathiri nakufanya huduma rafiki.

Mollely amesema Kubwa nikuongeza hali ya Usalama kwa watalii na kuongezwa vituo vya upimaji WA covid-19 kwa haraka katika hifadhi kuanzia mgeni anapoingia Nchini kufuata taratibu za kiafya na kutokuwa kinyuma na miongozo ya Shirika la Afya duniani ILi nikuhakikisha wakati mmoja watu zaidi ya 20 wanaweza kupata huduma

Aidha amesema kwa kushirikiana na watu wa wizara ya maliasili na Utalii wataweza kukaa kwa pamoja kuja na mikakati ya pamoja kwa kuwasiliana na Zanzibar kuwa na Mfumo mmoja wa uratibu ILi biashara za Utalii zisiharibike kwani suala la Afya nila muhimu pande zote hususani kwenye viwanja vya ndege na mipaka ya Tanzania.

Dr mollely amesema Wizara ya Afya ni sehemu ya nchi amewaomba walengwa waliopo kwenye viwanja vya ndege kuwasilikiliza vizuri Wafanyabiashara,watalii wanaotoka nje kuja Tanzania kulipia Huko huko ILi pindi mgeni anapongia Nchini wasikae zaidi ya dakika 45 lengo nikuhakiisha wageni waliopo nje hawaleti tatizo Nchini.

Naibu waziri wa Afya, Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kufanya Ziara katika uwanja wa ndege Kilimanjaro (Picha na Jane Edward Michuzi TV,) Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...