JESHI la Polisi kitengo cha Usalama barabarani, limetoa mafunzo kwa mafundi magari waliyokuwa ndani ya Kituo cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi Luis, Dar es Salaam kwa lengo la kuwafundisha namana ya kutambua vifaa ambavyo vipo kwenye magari hayo.

Mafunzo hayo yalitolewa kwa siku mbili na Mkuu wa Usalama Barabarani, ASP Ibrahim Samwix kwa lengo la mafundi hao kutambua mfumo wa injini ya gari unavyofanya kazi ili kuwarahisishia namna ya utengenezaji wa magari.

Pia,Mkuu huyo aliwafundisha kuhusu kifaa cha aina ya turbo kinavyofanya kazi, na namna ya kukitambua kama kikiwa kibovu, kwa sababu mafundi wengi wamekuwa wakifanya masuala ya ufundi kwa mazoea.

ASP Samwix alitoa pia mafunzo katika kifaa cha mfumo wa rejeta namna kinavyofanya kazi, kwa sababu mafundi wengi na madereva wamekuwa wakishindwa kutunza mabasi wanayopewa kutokana na mapungu madogo madogo.

Kabla ya mafunzo hayo, Mkuu huyo alianza na madereva kwa kuelimisha jinsi ya kufuata sheria za barabarani na kuendesha gari kwa mwendo ambao unatakiwa ili kuepusha ajali na kuokoa maisha ya wananchi.

Kwa wa upande wa madereva hao ambao walikuwa zaidi ya 40, walilishukuru Jeshi la Polisi kwa mafunzo hayo, kwa sababu yanawakumbusha kufuata sheria za barabarani, kutokana na kwamba wengi wanafanya kazi hiyo kwa mazoea.

Pia, wanasema ni mara yao ya kwanza kupatiwa mafunzo, kwa hiyowao wameona ni bahati kubwa kwa sababu wamejifunza mambo mengi kwa wakati mmoja kwa sababu wakati mwingine wanahisi kuwa wamesahaulika.

Aidha wameomba elimu hiyo na mafunzo hayo yawe endelevu kwa manufaa yao na kwa manufaa ya watumiaji wa barabara, wao wapo tayari muda wowote na pia wataendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.

Kwa upande wa abiria, Athuman Omary ambae ni Mkazi wa Tabata, Dar es Salaam alitoa shukrani kwa jeshi hilo kwa elimu ambayo walikuwa wanaitoa kwa dereva na wamiliki wa mabasi kwa sababu inaonesha ni jinsi gani wanajali maisha ya abiria.

Pia, Mkazi wa Ubungo, Mwajuma Juma aliwata madereva hao kutumia mafunzo waliyoyapa kwa kupunguza ajali za usalama barabarani kwa sababu kuna baadhi ya madereva hawafuati sheria hizo kwa makusudi.

Wakati huo huo wawamiliki wa mabasi, wamelipongeza jehi hilo kwa mafunzo ambayo wamepewa madereva wao pamoja na mafundi wa mabasi, wanasema hiyo itaondoa ajali za barabarani, itasaidia ulinzi wa magari yao na pia ushirikiano baina ya askari na wao utakuwa wa manufaa.


Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli Mbezi Luis Dar es eslaam, ASP Ibrahim Samwix akizungumza na mafundi wa magari waliyokuwa ndani ya Kituo cha Mabasi cha kwa lengo la kuwafundisha namna ya kutambua vifaa ambavyo vipo kwenye magari hayo.
Mafunzo hayo yalianza kutolewa Mei 27 mpaka Mei 28, 2021 jijini Dar es Salaam


Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli Mbezi luis Dar es eslaam ASP Ibrahim Samwix akiendelea na kazi kama anayoonekana pichani(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. You have given very good information, I thank you very much, this information is very helpful for me, that is why I have created this kind of information which is almost the same if you also want this kind of information. If someone reads, you can visit the majdashopping website for this and can read very easily through them.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...