Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ujambazi na uhalifu katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema wanaofanya hivyo waache kupima kina cha maji.
Ametoa onyo hilo leo Mei 7,2021 wakati anazungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungmzia umuhimu wa kuendelea kulinda amani na usalama nchini.
"Tumeahidi kudumisha amani na usalama, kama wazee mlivyotuomba na hili tutasimia kwa nguvu zote.Leo nimesoma habari sio kwenye mitandao ya kijamii, wanajaribu kina cha maji, Dar naomba nitoe meseji wasijaribu kina cha maji, na katika mitandao ile kuna kamanda ametajwa kuwa alikuwepo hapa Dar lakini ameondolewa.
"Mkuu wa Jeshi la Polisi uko hapa naomba hili ulifanyie kazi kuhusu huyo ambaye anatajwa kuwa alifanikiwa kudhibiti ujambazi.Lakini turudi tena kwenye mila desturi zetu kwani hali ngumu za uchumi haifanyi mtu awe jambazi, hivyo turudi tena kwenye maadili ya watoto wetu.Tusimamie hili kwa nguvu zote,"amesema Rais Samia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 07 Mei, 2021katika Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...