Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MKUU
wa Mkoa wa Pwani,Aboubakar Kunenge,, ametoa onyo kwa watendaji wa Bodi
ya Maghala na Wakala wa Vipimo ,mkoani humo, kushindwa kupima mizani
zilizopo kwenye maghala ya vyama vya Msingi zinazotumika kupokelea Ufuta
na kushindwa kusimamia maandalizi ya Maghala Makuu, hali
inayosababisha kero na kusuasua kwa zao hilo.
Alitoa onyo hilo,wakati akiendesha Mkutano wa Wadau wa Ufuta,Ikwiriri Wilayani Rufiji.
Kunenge alikerwa na watendaji hao wa Serikali kusubiri kuitwa na Wakulima badala ya kuwafuata na kutoa huduma.
Alieleza ,hahitaji kuona ubabaishaji,kwani hatosita kuwaondoa kwa kushindwa kusimamia wajibu wao kikamilifu.
Aidha
Kunenge alitoa muda wa Siku tatu kwa watendaji hao ,kuhakisha kuwa
wanakamilisha maandalizi ya Maghala Makuu na Upimaji wa Mizani kwenye
maghala ya Msingi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...