Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo May 24 ameanza rasrmi majukumu yake kwa kukutana na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam ambapo ameweka utaratibu wa kufanya kikao nao kila baada ya miezi mitatu.


RC Makalla amesema anatambua hamani na Mchango wa Wazee Katika jamii hivyo ameona ni vyema kuanza majukumu yake kwa kukutana nao ili kuchota busara na Baraka zao kwani anatambua Wazee ni hazina Muhimu.

Aidha RC Makalla amesema Katika kutatua kero na changamoto za Wananchi amepanga kuanza ziara ya utatuzi Kata kwa Kata hivyo amewahakikishia wananchi kuwa anayo dhamira ya dhati kuzipatia majibu kero zao.

Hata hivyo RC Makalla amesema kwakuwa Mkoa wa Dar es salaam ni Mkoa mkubwa na Wenye kutoa taswira ya nchi nzima kwenye kila nyanja mbalimbali, amejipanga kuhakikisha Jiji linakuwa shwari na watu wanafanya shughuli zao pasipo usumbufu wowote Kama maono na mategemeo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wao Wazee walioshiriki kikao hicho kwanza Wamemshukuru na Kumpongeza RC Makalla kwa namna anavyoheshimu Wazee na wamemuahidi kumpatia ushirikiano wa kutosha Katika majukumu yake.

Aidha Wazee hao wamesema Wana Imani kubwa na RC Makalla kwakuwa *wasifu wake wa uongozi unaonyesha kila alipopita amekuwa akiacha alama hivyo wanaamini atafanya Mambo makubwa na Mazuri Katika Mkoa wa Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...