Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MKUU
wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti amewataka wazazi na walezi wa
wanafunzi wa shule ya msingi Tanzanite ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara, kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha wanafunzi
wanakula chakula cha mchana shuleni hapo.
Mkirikiti
ameyasema hayo alipofanya ziara ya kutembelea shule hiyo na kukagua
ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu saba ya vyoo.
Amesema
wazazi na walezi wa shule hiyo wanapaswa kuhakikisha wanatimiza
majukumu yao kwa wanafunzi hao kwani serikali imeshatekeleza wajibu wake
kupitia elimu bila malipo.
“Chakula
wanachokula nyumbani hawa wanafunzi ndicho hicho ambacho wanakula
shuleni, hivyo wazazi na walezi wahakikishe wanatekeleza wajibu wao
kwani sisi serikali tumeshatimiza majukumu yetu,” amesema Mkirikiti.
Amesema
wazazi na walezi ambao watakuwa kikwazo cha kutimiza hilo apewe taarifa
zao ili aweze kuwachukulia hatua kwani wanafunzi wanapokuwa wanakula
shuleni kiwango cha taaluma huongezeka.
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Tanzanite, Anociatha Salla akisoma taarifa ya
shule hiyo amesema ina wanafunzi 1,016 wakiwemo wavulana 518 na
wasichana 498 wakitumia vyumba sita kwa uwiano wa wanafunzi 169 kwa
chumba kimoja cha darasa.
Mwalimu
Salla amesema kwa mujibu wa sera ya mwaka 1995 inaelekeza chumba kimoja
kwa wanafunzi 45 ila vyumba viwili vinavyojengwa vitapunguza kwa kiasi
changamoto ya madarasa.
“Tunapongeza
jitihada za mheshimiwa diwani wa kata ya Mirerani Salome Mnyawi na
nguvu za wananchi kujenga vyumba viwili vya madarasa na serikali
kumaliza na pia tunaanza msingi wa madarasa mengine,” amesema mwalimu
Salla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...