Taasisi ya Ustawi wa Jamii anawakaribisha wahitimu wote wa kidato cha sita na kidato cha Nne pamoja na wazazi wa wahitimu kwenye banda la Taasisi hiyo
katika maonyesho ya vyuo vikuu vya Elimu ya juu vya ufundi stadi.

Taasisi hiyo inashiriki Maonyesho hayo kwa mara ya pili sasa na mara hii Taasisi imejipanga kutoa huduma na elimu papo hapo.

Huduma zitolewazo kwenye Banda la Taasisi hiyo ni pamoja na udahili wa wanafunzi wapya, Ushauri wa Masuala ya Ndoa na Mahusiano, Elimu ya jinsia katika ajira pamoja na Sheria,haki na wajinu wa Mwajiri na Mwajiriwa .

 Maonyesho hayo ambayo yalianza tarehe 27 Mei na kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwq tarehe 28 yanaendelea mpaka tarehe 2 Juni.

Mhadhiri Msaidizi kutoka idara ya Taaluma za kazi (Labour Studies) Sarah Mbasha (Aliyeshika kipeperushi ) akifafanua jambo kuhusu kozi zinazotolewa na Taasisi kwa Wateja waliofika katika banda la Taasisi ya Ustawi wa Jamii kupata elimu na huduma Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Askari Polisi kikosi cha Usalama barabarani wa Mkoa wa Dodoma katika picha ya Pamoja na Mhadhiri Msaidizi kutoka  idara ya Ustawi wa Jamii taaluma Catherine Manda pamoja na Mhadhiri kutoka idara ya menejimenti ya rasilimali watu taaluma Dkt. Charles Ngirwa baada ya kupata elimu na huduma katika banda la Taasisi ya Ustawi wa Jamii uwanja wa Jamhuri Dodoma
Mhadhiri wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii idara ya Menejienti ya Rasilimali watu Dkt. Charles Ngirwa akimuhudumia mteja aliyefika katika Banda la Taasisi kupata huduma.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...