Kiungo bora wa timu ya Iringa All Stars Veterens Steve Lihawa akiwachambua wachezaji wa timu pinzani wakati wa bonanza la Iringa veterans Combine

Kiungo bora wa timu ya Iringa All Stars Veterens Ally Msigwa akimtoka mchezaji wa timu pinzani wakati wa bonanza la Iringa veterans Combine
Kikosi cha Timu ya Iringa All Stars Veterens kilichoibuka mabingwa wa bonanza la Iringa veterans Combine
wachezaji wa Timu ya Iringa All Stars Veterens wakishangilia ubingwa mbele ya kiungo wa timu ya Iringa Veterans
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Timu ya Iringa All Stars
Veterans imeibuka bingwa wa Bonanza la Iringa Combine Veterani kwa kuifunga
timu ya Iringa Veterans kwa goli moja bila katika uwanja wa kumbukumbu ya
Samora lililokuwa limeshirikisha jumla timu sita za veteran mkoani Iringa.
Timu ya Iringa All Stars
Veterans ilianza kwa kuifunga timu ya Ruaha stars Veteran kwa jumla ya magoli
mawili kwa bila(2-0) na mchezo wa pili ulikuwa kati ya Timu ya Iringa All Stars
Veterans na Ilula Veteran na timu ya Timu ya Iringa All Stars Veterans ilibuka
na ushindi wa goli nne kwa bila (4-0) na kuipeleka timu hiyo moja kwa moja
katika hatua ya fainali.
Katika hatua ya fainali ya
Bonanza la Iringa Combine Veterani timu ya Iringa All Stars Veterans imeibuka
bingwa wa Bonanza la Iringa Combine Veterani kwa kuifunga timu ya Iringa
Veterans goli moja kwa bila(1-0), goli lililofungwa na kiungo machachali wa wa
timu hiyo anayejulikana kwa jina la Omary Albert aliyeingia kipindi cha pili
akitokea bench kuchukua nafasi ya Ramadhan Shemuhilu.
Katika bonanza hilo timu ya
Iringa All Stars veterans iliibuka bingwa katika idara zote kwa kumtoa mfungaji
bora wa bonanza hilo Ramadhan Shemuhilu kwa kufunga jumla ya magoli matatu huku
akifuatiwa na Omary Albert aliyefunga magoli mawili,kwa upande wa mchezaji bora
wa bonanza hilo, timu ya Iringa All Stars veterans ilitoa tena mchezaji bora wa bonanza hilo anayejukana kwa jina
Steve Lihawa maarufu (Iniesta).
Katika bonanza hilo timu ya
Iringa All Stars Veterans ilikuwa timu
iliyokuwa inamvuto kwa kupiga pasi nyingi kwa uelewano maarufu kama kampa kampa
tena jambo ambalo liliwafanya mashabiki na baadhi ya wachezaji wa timu nyingine
kuvutiwa na kiwango cha timu hiyo.
Hata hiyo haikuwa kazi rahisi
kushinda ubingwa huo kwa kuwa timu kama Mafinga Veteran,Iringa Veterani na
Ruaha stars veteran walikuwa wanawachezaji ambao kwa kiasi kikubwa walionyesha
kandada safi uwanjani.
Kwenye mchezo wa fainali baina
ya timu ya Iringa All Stars Veterans Na Iringa Veteran kulikuwa na ushindani
katika eneo la kiungo ambalo kwa timu ya Iringa All Stars Veterans walikuwa na
viungo watatu ambao ni Ally Msigwa,Winfredy Fyataga na Steve Lihawa na baadae
aliongezeka Ally Luambano kiasi kwamba walifanyikiwa kukivuruga kiungo cha timu
ya Iringa Veteran kilichokuwa chini ya Alex Mbewe na wenzake.
Wakizungumzia bonanza hilo
baadhi ya wachezaji walioshiri waliwapongeza timu ya Iringa All Stars Veterans kwa
kuwa mabingwa na kutoa sifa kede kede kwa waandaji wa bonanza hilo ambalo
lilikuwa kubwa na liliwavutia watu wengi
Naye kepteni wa timu ya Iringa
All Stars Veterans Lissa Mwalupindu alisema kuwa wamelitumia bonanza hilo kwa
ajili ya kujiandaa na bonanza la kitambi Noma litakalofanyika mwishoni wa wiki
hii jijini Arusha
Kwa upande wake Katibu mkuu wa
umoja wa veteran mkoa wa Iringa na mratibu wa bonanza hilo Pastory Kwambiana
alisema kuwa lengo la bonanza hilo ni kuleta umoja na mshikamano kwa wachezaji
wa zamani na kuwa kitu kimoja katika kukuza na kuinua soka la mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa umoja wa maveteran
mkoa wa Iringa umedhamilia kuona heshima ya soka inarudi mkoani Iringa kwani
wamepanga kuwa na utaratibu wa kuvitembelea vilabu ili kubadilishana mawazo
yatakayoisaidia timu.
Bonanza la Iringa Combine Veterani,
limeshirikisha timu sita ambazo ni Iringa veterans, Mkwawa veterans, Ruaha
veterans, Mafinga Veterans Ilula veterans na Iringa All Stars Veterans
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...