Uongozi wa Chama cha Skauti Tanzania umetakiwa kuwafinyanga vijana kiuzalendo ili kuwajenga maadili mema yatakayowawezesha kupiga vita vitendo viovu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo alipokutana kwa mazungumzo na uongozi wa Chama hicho uliofika Ofisini kwake Vuga jijini Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kuwa mafunzo ya skauti ni eneo muhimu kwa maslahi ya taifa kutokana na mchango wake mkubwa katika kuwajengea maadli mema vijana sambamba na kuwapatia elimu ya ubunifu.

Aidha amesema kuna haja kwa uongozi wa Skauti Tanzania kuwafunza vijana namna bora ya kuweza kutambua ubaya na kupinga rushwa, ubadhirifu pamoja na uhujumu wa uchumi.

Akigusia suala la mashirikiano Mhe. Hemed ameuhakikishia uongozi huo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa ushirikiano wake, katika kuhakikisha mchango wa chama hicho unatambulika Nchini.

“Jamii lazima itambue kwamba kazi ya kuwalea vijana si ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Chama hicho pekee, bali ni jukumu la  jamii kwa ujumla.

Nae  Makamu mwenyekiti wa chama hicho ambae pia ni waziri wa elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohamed Said alisema Wizara anayoisimamia itahakikisha wanawapa mashirikiano ya uongozi wa Skauti Tanzania kwa lengo la kusimamia utendaaji kwa vijana wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Pamoja na mjabo mengine Mhe. Simai alieleza kuwa Chama cha Skauti kwa upande wa Zanzibar kimeimarika vyema katika kusaidia malezi bora katika jamii.

Mapema akitoa taarifa kwa Makamu wa Pili wa Rais Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mwantum Bakari Mahiza alisema chama hicho kwa upande wa Zanzibar kina zaidi ya miaka 109 tangu kuanzishwa kwake ambapo kimekuwea kikipata mashirikiano mazuri kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Kiongozi huyo alimueleza Mhe. Hemed kuwa hivi sasa uongozi wa Skauti unajenga kambi ya kimaitaifa Makao Makuu ya Nchi Jijini Dodoma hivyo alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali ya Mapinduiz ya Zanzibar kuwapatia eneo maalum kwa ajili ya kujenga chuo cha kutolea mafunzo kwa vijana.

Chama cha Skauti Nchini Tanzania kina jukumu la kulea na kuwafunza nidhamu na maadili mema, ukakamavu kwa vijana wa kitanzania kwa taasisi mbali mbali za SMT na SMZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdula akizungumza na uongozi wa Chama cha Skauti Tanzania ukiwa pamoja na Uongozi wa wizara ya Elimu na Mafunzo Amali uliofika Afisini kwake Vuga kubadilishana nae mawazo juu ya utendaji wa kazi wa chama hicho.
Mhe. Hemed Suleiman Abdula kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chama cha Skauti Tanzania ukiwa pamoja na Uongozi wa wizara ya Elimu na Mafunzo Amali mara baada ya mazungumzo yao.Picha na – OMPR – ZNZ.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...