WANANDOA, raia wa India, Devang Josh (42) na Belaben Prajapati (47), wamehukumiwa kulipa faini ya Shilingi milioni moja au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada ya kukiri kosa la kuishi nchini bila kibali na kumsaidia mke wake kuishi nchini wakati akijua ni muhamiaji haramu.

Hukumu hiyo, imesomwa leo Mei 25, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya washtakiwa kukiri makosa yanayowakabili.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Shaidi amesema, katika shtaka la kwanza la kuishi nchini bila kibali mshtakiwa Prajapati, atatakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 na akishindwa atatumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani huku katika shtaka la pili linalomkabili Josh, Mahakama imemkuta na hatia kwa hiyo atatakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 au akishindwa atatumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani.

Mapema kabla ya hukumu, mahakama iliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ndipo Wakili wa Serikali kutoka Idara ya Uhamiaji, Godfrey Njwijo aliiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kutenda makosa kama hayo.

Hata hivyo, mpaka muda wa Mahakama unakwisha, washtakiwa hao hawakuweza kufanikiwa kulipa faini hiyo na wamepelekwa gerezani kwa ajili ya kuanza kutumikia vifungo vyao.

Awali ilidaiwa, Mei 21,2021 mshtakiwa Prajapati peke yake

akiwa katika eneo la Kariakoo ndani ya Mkoa wa Dar es Slaam akiwa raia wa India alikutwa akiishi nchini bila kibali. Pia alikutwa akiishi ndani ya Jamhuri y Muungano wa Tanzania bila Visa halali au nyaraka nyingine yoyote inayomruhusu kufanya hivyo.

Katika shtaka la pili, unadaiwa mshtakiwa Josh anatuhumiwa tarehe hiyo hiyo na eneo hilo alipokutwa mshtakiwa Prajapati, alimsaidia mke wake huyo ambae ni muhamiaji haramu kuishi nchini bila Visa wakati akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...