KUELEKEA Uzinduzi wa Miss Kagera 2021 washiriki wa Shindano hilo kwa Wilaya ya Biharamulo, wamejitokeza hadharani mbele ya Mashabiki zao na kufanya Usafi eneo la Stendi ya Mabasi Biharamulo Mjini.
Wakiongea na Michuzi TV kwa Nyakati tofauti eneo la Stendi washiriki hao wameonekana kufurahishwa na programu hiyo ambayo imeandaliwa na Waandaaji ikiwa na lengo la kuwasogeza karibu na jamii, lakini ujumbe ukiwa Ni Jamii kuona suala la umuhimu wa kutunza Mazingira kwa Kufanya Usafi maeneo yao.
Ijumaa hii ndiyo siku pazia la Miss Kagera linafunguliwa ambapo Shughuli inaanzia Biharamulo kisha Ngara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...