Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi wakimsikiliza Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Khalifa Abdulrahman Almazrzouqi wakati wa kikao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambapo wamezungumzia mikakati ya kukuza Utalii nchini ikiwemo kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo nchini katika ndege za Emirates na vyombo vya habari vya kimkakati vilivyopo Uarabuni ili kuteka soko la Utalii katika Umoja wa Falme hizo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akimsikiliza Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Khalifa Abdulrahman Almazrzouqi kbala ya kuagana mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaa ambapo wamezungumzia mikakati ya kukuza Utalii nchini ikiwemo kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo nchini katika ndege za Emirates na vyombo vya habari vya kimkakati vilivyopo Uarabuni ili kuteka soko la Utalii katika Umoja wa Falme hizo.

Waziri wa Maliasil na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Menejimenti ya NMB makao makuu katika kikao kilichofanyika leo mapema Jijini Dar es Salaam kilicholenga kuboresha mahusiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Benki hiyo ili kufanya kazi kwa pamoja katika kutangaza vivutio vya utalii nchini kwa kuwawezesha kufanya malipo kupitia Benki hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...